Shairi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'mashairi huweza kuandikwa au kutungwa kulingana na jinsi yanavyoonekana. hii ina maana kuwa, mashairi huweza kutofautishwa kwa idadi ya mishororo, jinsi maneno ...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 10:29, 8 Septemba 2012

mashairi huweza kuandikwa au kutungwa kulingana na jinsi yanavyoonekana. hii ina maana kuwa, mashairi huweza kutofautishwa kwa idadi ya mishororo, jinsi maneno yalivyopangwa, urari wa vina na kadhalika. AINA ZA MASHAIRI KUTOKANA NA IDADI YA MISHORORO 1. TATHNIA/UWILI shairi hili huwa na mishororo miwili katika kila ubeti. vina vyake vyaweza kuwa na mtiririko. 2. TATHLITHA/UTATU shairi hili huwa na mishororo mitatu katika kila ubeti. vina vyake huenda vikawa na urari. 3. TARBIA shairi la aina hii huwa na mishororo minne katika kila ubeti. mara nyingi shairi hili hugawanywa katika sehemu mbili, ukwapi na utao. mshororo wa kwanza wa shairi hili huitwa kipokeo, wa pili huitwa mloto, wa nne huitwa kibwagizo. kibwagizo huwa kinarudiwarudiwa katika kila ubeti. 4. TAKHMISA hili ni shairi lenye mishororo mitano katika kila ubeti 6. TASDISA shairi hili huwa na mishororo sita katika kila ubeti 7. TATHMINA hili ni shairi lenye mishororo minane katika kila ubeti 8. UKUMI ukumi ni shairi lililo na mishororo kumi katika kila ubeti

AINA ZA MASHAIRI JINSI YANAVYOJITOKEZA 1. KIKWAMBA kikwamba ni aina ya shairi lililo na kibwagizo ambacho ni kifupi ukilinganisha na ile mishororo mingine. hili huweza kuuchukuwa mfumo wa mashairi yale mengine. 2. HURU/GUNI/VUE shairi huru/guni au vue huwa ni shairi ambalo halifuati sheria za kiarudhi. hili hutungwa tu kikawaida. 3. NGONJERA shairi hili huhusisha waimbaji zaidi ya mmoja. uimbaji wao huwa katika mfumo wa majibizano.