Tofauti kati ya marekesbisho "Wapangwa"

226 bytes added ,  miaka 8 iliyopita
no edit summary
'''Wapangwa''' ni kabila kutoka [[Milima Livingstone]] karibu na pwani ya mashariki ya [[Ziwa Nyasa]], [[wilaya ya Ludewa]], [[Mkoa wa Njombe]], kusini ya nchi ya [[Tanzania]]. Mwaka 2002 idadi ya Wapangwa ilikadiriwa kuwa 150,000.
 
Chakula chao ni [[ugali]] wa [[mahindi]], [[ulezi]] na [[mtama]] kidogo. Kitoweo cha vyakula hivyo ni [[maharage]], samaki, [[nyama]] na jamii ya mboga mboga. Kinywaji chao ni pombe (ukhimbi) yaani kangala, komoni, [[ulanzi]] ambao hugemwa kutoka katika mmea uitwao mlanzi. Pia Wapangwa ni hodari sana kwa utegaji na uwindaji wa wanyama pori kama vile ( kwa lugha yao)
Nyhaluchi,mahtu ngwehe, sudi,ng'ese,ng'wali ni videke.
 
Hulima mazao mbalimbali ya chakula katika maeneo ya miinuko na mabondeni kandokando ya mito.Hulima Nikwa ushirika unaoitwa njhiika.Pia ni wafugaji wa makundi madogomadogo ya [[ng'ombe]], [[mbuzi]], [[kondoo]] na [[nguruwe]] (kitimoto). Pia hulima mazao ya biashara kama [[kahawa]], [[chai]], [[pareto]], [[mahindi]]. Kabila hili pia hupata matunda ya asili kama vile; masada, savula, makuhu, mahofita,mafudo, minhingi, vudong'o na nisongwa.
Usafiri wao wa asili ni kwa chombo kiitwacho ngwichili ambacho kinatengenezwa kwa kutumia miti asilia.
Nyumba zao za asili kwa sasa ni za matofali ya udongo ya kuchoma na kuezekwa kwa bati, hata hivyo nyumba zao za asili zinajengwa kwa kutumia miti asili kugandikwa kwa udongo wa mfinyanzi na kuezekwa kwa nyasi aina ya hunji na lihanu.
 
Mavazi yao ya asili ni nguo zilitengenezwa kwa ngozi za wanyama pamoja na magome ya miti ya misambi ambayo hupondwapondwa,hufumwa na kupakwa mono.
 
Lugha yao ni [[Kipangwa]].
Anonymous user