NATO : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 3:
'''NATO''' ni kifupi cha '''North Atlantic Treaty Organisation''' au '''Jumuiya ya Mkataba wa Atlantiki ya Kaskazini''' ambayo ni ushirikiano wa kujihami ya kambi ya magharibi. Inaunganisha nchi nyingi za [[Ulaya]] pamoja na [[Marekani]] na [[Kanada]]. Nchi wanachama zimeahidi kuteteana kama moja inashambuliwa na nje. Makao makuu yapo [[Brussels]].
 
NATO ilianzishwa mwaka 1949 wakati wa [[vita baridi]] kama maungano ya nchi za Ulaya ya magharibi pamoja na Marekani dhidi ya [[Umoja wa Kisovyeti]] na nchi shiriki zake katika [[Mapatano ya Warshawa]]. Nchi wanachama wa kwanza walikuwa [[Marekani]], [[Ubelgiji]], [[Uholanzi]], [[Luxemburg]], [[Ufaransa]], [[Uingereza]], [[Kanada]], [[Ureno]], [[Italia]], [[Norwei]], [[Denmark]] na [[Iceland]]. 1952 [[Ugiriki]] na [[Uturuki]] zilijiunga pia zikafuatwa na [[Ujerumani ya Magharibi]].
 
Baada ya mwisho wa vita baridi nchi zilizokuwa chini ya Umoja wa Kisoveti kama sehemu ya kambi ya kikomunisti zilijiunga na NATO kuanzia mwaka 1999. Ndizo Hungaria, [[Ucheki]], [[Poland]] (1999), halafu [[Estonia]], [[Latvia]], [[Lithuania]], [[Slovenia]], [[Slovakia]], [[Bulgaria]] na [[Romania]] (2004).