Kalenda ya mwezi : Tofauti kati ya masahihisho
Content deleted Content added
No edit summary |
No edit summary |
||
Mstari 1:
[[Kalenda ya mwezi]] inahesabu miezi kufuatana na mwendo wa mwezi. Mwezi una muda wa siku 29,5 kutoka mwezi mpya hadi mwezi mpya. Faida yake ni ya kwamba mwezi unaonekana na watu wote. Hali hii inasaidia kuelewana haraka kati ya watu juu ya tarehe fulani katika mazingira ambako hakuna mitambo wala maandishi. Mwaka wa miezi hii 12
Kwa sababu hiyo [[kalenda]] za kale katika mataifa na tamaduni mbalimbali mara nyingi zilikuwa hasa kalenda za kufuata mwezi.
Kutokana na sababu hizo kalenda za mwezi zilirekebihswa mara nyingi kwa njia ya kuingiza siku za nyongeza ili muda wa mwaka ilingane na mwaka wa jua.
[[Kalenda ya Kiyahudi]] ni mfano hadi leo jinsi mwaka wa mwezi unasahihishwa kwa kuingiza miezi ya nyongeza. Katika utaratibu wa kipindi cha miaka 19 kuna miaka 12 ya kawaida na miaka saba yenye mwezi wa nyongeza inayobadilishana ili kulinganisha kalenda ya mwezi na mwendo wa jua hivyo mwezi wa mavuno inabaki katika majira yake.
Kalenda ya mwezi tupu ambayo ni muhimu hadi leo ni [[kalenda ya kiislamu]]. Tarehe zake zinabadilika kila mwaka katika [[kalenda ya Gregori]] ambayo ni Kalenda ya kimataifa. Kwa mfano [[Ramadhani]] iko mwaka 2006 BK wakati wa Novemba; kila mwaka inasogea mbele itafika miezi ya Agosti, Mei, Januari na kadhalika hadi kurudi tena Novemba katika mwendo wa miaka wapitao 33.
{{mbegu}}
|