Western : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Spaghetti Westerns
 
No edit summary
Mstari 1:
'''Western''' (kutoka [[kiing.]] "West" - ''magharibi'') ni aina ya filamu yenye asili katika [[Marekani]]. Western husimulia hadithi za watu walioishi wakati wa [[karne ya 19]] hadi mwanzo wa [[karne ya 20]] Marekani ilipoenea katika sehemu za magharibi ya [[Amerika ya Kaskazini]]. Filamu kuhusu kipindi hiki zhilianza kupatikana tangu mwanzo wa karne ya 20.
#REDIRECT [[Spaghetti Westerns]]
 
Kazi muhimu ya filamu hizi ilikuwa kuwapa watu wa Marekani picha kuhusu historia yao na kuhusu tabia nzuri ya mababu walioanzisha na kueneza taifa yao. Ukweli wa kihistoria jinsi ilivyo katika hadithi za kitaifa ilibaki nyuma mara nyingi.
 
Filamu za Western zilitengenezwa baadaya pia Ulaya kama aina ya [[Spaghetti Western]] na mara nyingi zilicheza na aina za wahusika jinsizilivyokuwa kawaida katika filamu za Marekani.
 
==Mazingira ya kihistoria ya filamu hizi==
Katika nyakati zile Marekani ilitawala tu sehemu za mashariki za Amerika ya Kaskazini na kupanua polepole kuelekea magharibi hadi kufikia Pasifiki na baadaye pia kutawala maeneo ya katikati. Palikuwa na eneo la "mpakani" (''frontier'') ambako wakulima walowezi na wafugaji kutoka Marekani waliingia katika nchi ya wakazi asilia au [[Maindio]] na kuanzisha makazi yao huko. Mashamba na miji yale yalikuwa nje ya eneo la Marekani yenyewe. Kwa hiyo maisha yalikuwa kwa muda bila sheria wala serikali. Hata kama maeneo mapya yaliingizwa katika [[Maungano ya Madola ya Amerika]] taasisi za serikali zilikuwa mbali kwa muda na kazi ya kuratibu maisha ilibaki mkonono wa watu wenyewe katika eneo fulani.
[[Image:Buffalo Bill's Wild West Show.jpg|thumb|300px|Macowboy kazini]]
==Wahusika katika hadithi za Western==
Hadithi zinazosimuliwa katika filamu za western mara nyingi huwa na watu wafuatao:
* '''Cowboy''' au mchunga ng'ombe - anayeonyeshwa mara nyingi kama mtu mwenye kazi ngumu asiye na elimu lakini ni hodari. Kwa kawaida ni mtu mwema.
* '''Sheriff''' au mpolisi - anayepigana na waovu anayelala ofisini mwake anapoangalia wafungwa. Kazi yake ni pia kutetea wafungwa kama watu wa mji wanataka kuwanyonga mara moja. Kwa kawaida ana uwezo wa kutumia bunduki yake haraka sana. Huwa ni mtu mwema
* '''Rancher''' au mwenye shamba la mifugo - yeye ni mwajiri wa macowboy. Ama ni mtajiri sana au yeye ni maskini anayeanza kujenga maisha yake na kupambana na matatizo ya kila aina. Mara nyingi ni mtu mwema lakini hutokea pia kama mbaya anayetaka kujitajirisha hata akimwua jirani
* '''Watu wa mjini''' - ama mwenye duka au mwenye kilabu. Anahofia waovu wanaopita mjini na kupora pesa zake. Kwa kawaida huwa mwoga asiye tayari kumsaidia sheriff.
* '''Undertaker''' au mzishi ni mtu wa mjini wa pekee anayefurahia kila maiti inayoongeza mapato yake. Kwa hiyo hana neno na waovu na kwa kawaidi hawana neno naye. Asipokuwa na nafasi ya pembeni kabisa katika hadithi yeye huwa ni mwanafalsafa wa filamu mwenye hekima nyingi kuhusu maisha na mauti.
* '''Mwanamke''' - aina yake ilikuwa haba huko magahribi ya kale kwa hiyo hakuna nafasi nyingi kwa waigizaji wa kike katika filamu za Western. Mwanamke hupatikana kwa namna mbili. Ama yeye ni mke wa rancher au wa mtu wa mjini, mcha Mungu na hodari akishika bunduki. Au yeye ni mwimbaji katiba kilabu anayedharauliwa na watu wa kawaida lakini macowboy humpenda; mara nyingi ni rafiki wa siri wa sheriff au mwovu mkuu anayeweza kumsaidia; hali halisi yeye ni mkahaba lakini filamu za Western za kawaida hawaonyeshi upande huu wa kazi yake waziwazi isipokuwa tangu kupatikana kwa [[Spagehtti Western]] upande huu wa maisha umeonyeshwa pia kiasi. Kazi muhimu ya mwanamke katika filamu hizi ni kuwapa wanaume sababu ya kupigana ama kwa mikono -hasa kilabuni wanapovunja viti vingi pamoja kioo chopo katikati ya rafu ya vyupa- au kwa bunduki. Hii ni sababu ya kwamba undertaker huwaheshimu wakinamama hata asipopata nafasi nyingi ya kuwazika.
*'''Mwanamke wa pekee''' ni binti wa rancher anayerudi kutoka masomoni. Alipoondoka alikuwa msichana mdogo lakini akirudi ni mrembo anayesababisha mvurugo kati ya wanaume wa eneo mara moja. Huingzwa hasa katika filamu pasipo na haja ya damu nyingi.
*'''Mwovu mkuu na wenzake''' ni pilipili na sukari ya filamu za Western. Wanafika kutoka nje na kuleta kifo mpaka wameuawa wenyewe. Mara wanashambulia benki mara wanafuata mipango ya kulipiza kisasi kwa sababu sheriff wa mji aliwahi kumwua kaka wa mwovu mkuu miaka 23 iliyopita. Wakati mwingine wameajiriwa na rancher mbaya kumfukuza jirani wake mwema kwa sababu chemchemi ya pekee iko ndani ya eneo lake. Wakati mwingine mwovu huonyeshwa kuwa na tabia nzuri kwa sababu ameshakata shauri kuacha maovu lakini kwa bahati mbaya tangazo lenye picha yake linalotangaza ya kwamba kuna pesa fulani kwa yeyote anayemkamata au kumwua liko katika ofisi ya sheriff. Kwa hiyo sheriff anapaswa kumwinda. Kama sheriff angependelea kutomwona kuna mwovu wa aina nyingine ni headhunter au mwindaji wa waovu wanotafutwa anayetaka kichwa chake kwa sababu ya pesa.
[[Image:The searchers Ford Trailer screenshot (25).jpg|thumb|300px|Macowboy na Maindio (bado hai)]]
*'''Mmeksiko''' ni mtu mdogo asiyeongea Kiingereza sanifu ni mtu anayestahili kupigwa na kudharauliwa na macowboy. Kosa lake ni ya kwamba miaka kadhaa iliyopita alishindwa na Waamerika na kubaki kwenye nchi iliyovamiwa na Marekani. Katika mawestern za baadaye mara chache anapata nafasi ya kumwua mwovu pia.
 
*'''Indio''' au mwenyeji asilia wa Amerika ni hatari. Anaiba mifugo na kushambulia ovyo wazungu wazuri Wamarekani. Kama mkurugenzi wa filamu amepewa pesa ya kutosha kwa kuajiri waigizaji wa kutosha maindio wengi sana hushambulia nyumba ya rancher au hata mji wote wakikaribia kushinda lakini kwa bahati nzuri cavallery (jeshi la farasi) hufika na kuwafukuza. Katika Western za baadaye hutokea ya kwamba sababu za Waindio zaelezwa kwa nini wanashambulia kwa mfano kwa sababu Wamarekani walitwaa ardhi yao au kuua watoto wao.
 
==Maajabu ya Western==
Tabia ya ajabu ya watu katika filamu hizi ni wakifika mjini baada ya kusafiri njia ndefu kwa farasi kwenye jua kali huingia mara moja kilabuni. Hapa hawanywi maji au angalau bia lakini mara moja pombe kali ya whiskey angalau chupa kimoja.
 
Tabia nyingine ya ajabu ni ya kwamba wakipigwa risasi hufa mara moja bila kulia. Huanguka tu na kuwa kimya. Hakuna wajeruhiwa wanaoendelea kulia kwa masaa mengi usiku wote. Wengine hawaagi dunia mara moja lakini huwa na hotuba kabla ya kufa.
Kuna pia aina nyingine wakipigwa risasi wanakata tu kipande cha shati na kufunika jeraha na kuendelea na mapigano bila matatizo.
 
[[Category:Filamu]]
[[Category:Marekani]]
 
[[ca:Western]]
[[cs:Western]]
[[da:Westernfilm]]
[[de:Western]]
[[en:Western (genre)]]
[[es:Western]]
[[eo:Vakera filmo]]
[[fr:Western]]
[[gd:Siar-sgeul]]
[[hr:Western]]
[[io:Armizita rebelo]]
[[is:Vestri]]
[[it:Western]]
[[he:מערבון]]
[[nl:Western (film)]]
[[ja:西部劇]]
[[no:Westernfilm]]
[[pt:Cinema western]]
[[ru:Вестерн]]
[[fi:Western]]
[[sv:Western]]
[[tr:Western]]