Western : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 15:
* '''Watu wa mjini''' - ama mwenye duka au mwenye kilabu. Anahofia waovu wanaopita mjini na kupora pesa zake. Kwa kawaida huwa mwoga asiye tayari kumsaidia sheriff.
* '''Undertaker''' au mzishi ni mtu wa mjini wa pekee anayefurahia kila maiti inayoongeza mapato yake. Kwa hiyo hana neno na waovu na kwa kawaidi hawana neno naye. Asipokuwa na nafasi ya pembeni kabisa katika hadithi yeye huwa ni mwanafalsafa wa filamu mwenye hekima nyingi kuhusu maisha na mauti.
* '''Mwanamke''' - aina yake ilikuwa haba huko magahribi ya kale kwa hiyo hakuna nafasi nyingi kwa waigizaji wa kike katika filamu za Western. Mwanamke hupatikana kwa namna mbili. Ama yeye ni mke wa rancher au wa mtu wa mjini, mcha Mungu na hodari akishika bunduki. Au yeye ni mwimbaji katiba kilabu anayedharauliwa na watu wa kawaida lakini macowboy humpenda; mara nyingi ni rafiki wa siri wa sheriff au mwovu mkuu anayeweza kumsaidia; hali halisi yeye ni mkahaba lakini filamu za Western za kawaida hawaonyeshi upande huu wa kazi yake waziwazi isipokuwa tangu kupatikana kwa [[SpagehttiSpaghetti Western]] upande huu wa maisha umeonyeshwa pia kiasi. Kazi muhimu ya mwanamke katika filamu hizi ni kuwapa wanaume sababu ya kupigana ama kwa mikono -hasa kilabuni wanapovunja viti vingi pamoja kioo chopo katikati ya rafu ya vyupa- au kwa bunduki. Hii ni sababu ya kwamba undertaker huwaheshimu wakinamama hata asipopata nafasi nyingi ya kuwazika.
*'''Mwanamke wa pekee''' ni binti wa rancher anayerudi kutoka masomoni. Alipoondoka alikuwa msichana mdogo lakini akirudi ni mrembo anayesababisha mvurugo kati ya wanaume wa eneo mara moja. Huingzwa hasa katika filamu pasipo na haja ya damu nyingi.
*'''Mwovu mkuu na wenzake''' ni pilipili na sukari ya filamu za Western. Wanafika kutoka nje na kuleta kifo mpaka wameuawa wenyewe. Mara wanashambulia benki mara wanafuata mipango ya kulipiza kisasi kwa sababu sheriff wa mji aliwahi kumwua kaka wa mwovu mkuu miaka 23 iliyopita. Wakati mwingine wameajiriwa na rancher mbaya kumfukuza jirani wake mwema kwa sababu chemchemi ya pekee iko ndani ya eneo lake. Wakati mwingine mwovu huonyeshwa kuwa na tabia nzuri kwa sababu ameshakata shauri kuacha maovu lakini kwa bahati mbaya tangazo lenye picha yake linalotangaza ya kwamba kuna pesa fulani kwa yeyote anayemkamata au kumwua liko katika ofisi ya sheriff. Kwa hiyo sheriff anapaswa kumwinda. Kama sheriff angependelea kutomwona kuna mwovu wa aina nyingine ni headhunter au mwindaji wa waovu wanotafutwa anayetaka kichwa chake kwa sababu ya pesa.