Wolverini : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d r2.7.3) (Roboti: Imeongeza vep:Hahm
No edit summary
Mstari 21:
''G. g. luscus''
}}
'''Wolverini''' (kutoka [[Kiingereza|Kiing.]]: ''[[w:Wolverine|wolverine]]'', Kisayansi: ''Gulo gulo'') ni mnyama wa familia ya [[Mustelidae]] mwenye nywele nyeusi na nyeupe za matimutimu.
 
'''Wolverini''' (kutoka [[Kiingereza|Kiing.]]: ''[[w:Wolverine|wolverine]]'', [[Kilatini|Kilat.]]: ''Gulo gulo''), pia huitwa '''mlafi''', '''karkajuu''' au '''dubu-kicheche''', ni spishi kubwa zaidi kati ya wanyama wanaoishi ardhini wa familia ya [[Mustelidae]] (cheche). Ni [[Carnivora|mla-nyama]] mnene mwenye misuli ambaye hufanana kwa karibu zaidi na [[dubu]] mdogo kuliko mustelidi wengine. Wolverini huwa wakatili na wenye nguvu nyingi kwa kuwiana na ukubwa wao, na huwa uwezo wa kuua mawindo yao makubwa zaidi kuwaliko.
[[Picha:Gulo_gulo_distribution.svg|thumb|left|Ramani inaonyesha maeneo yaliyokaliwa na wolverini (nyekundu)]]
 
Wolverini wanapatikana hasa katika [[taiga]] (biomu inayojulikana kwa kuwa na misitu ya [[mpia|mipia]], kama vile: [[mpaini|mipaini]], [[msprusi|misprusi]] na [[mlachi|milachi]]), maeneo ya chini ya Aktiki na [[tundra ya kialpu]] ya [[Nusudunia ya Kaskazini]] ambapo kuna wolverini wengi kaskazini mwa [[Kanada]], [[Alaska]] na [[nchi za Kinordiki]] za Ulaya, na [[Urusi|Urusini]] na [[Siberia]]. Idadi yao imepungua tangu karne ya 19 kutokana na utegaji, upunguzaji wa eneo na kuvunjavunja makazi yao, hivi kwamba huwa hawapatikani kabisa mwishoni mwa kusini mwa eneo lao la Ulaya. Idadi kubwa zinafikiriwa kubaki [[Amerika Kaskazini]] na Ulaya kaskazini. Wolverini huwa wanyama pweke.
{{mbegu-mnyama}}
 
{{Jaribio1| maneno_ya_asili = skunk-bear | lugha = Kiingereza | maneno_ya_jaribio = konje-dubu }}
== Taksonomia ==
Ushahidi wa kinasaba unadokeza kwamba wolverini huwa uhusiano kwa karibu zaidi na [[taira]] na [[konje]] (majina ya kisayansi ''Eira'' na Martes'').
 
Kati ya jenasi ya ''Gulo'', utengano hutokea kati ya spishi mbili za chini: spishi ya [[Dunia ya Kale]] ''Gulo gulo gulo'' na spishi ya [[Dunia Mpya]] ''G. g. luscus''. Mabingwa wengine wameelekea spishi wanne wengine za chini, kama wale wanaotegemea [[Kisiwa cha Vancouver]] (''G. g. vancouverensis'') na [[Peninsula ya Kenai]] katika Alaska (''G. g. katschemakensis''). Hata hivyo, taksonomia iliyopokewa kwa desturi inatambua spishi mbili za chini za bara au inatambua taksoni moja ya [[holaktiki]].
 
Ushahidi wa kinasaba uliokusanya karibuni unatambua kwamba wolverini wengi wa Amerika Kaskazini watokana na asili moja, labda kutoka [[Beringia]] wakati wa [[kipindi cha barafu]] cha mwisho na haraka walipanua baadaye, hata hivyo hii ni ngumu ya kujua kwa uhakika.
 
== Tabia za kimaumbile ==
Kimaumbile, wolverini huwa mnyama mwenye mwili mnene na misuli. Wao huwa na miguu mifupi, kichwa kipana cha mviringo, macho madogo na masikio mafupi. Wao hufanana kwa karibu zaidi na dubu kuliko [[Mustelidae|mustelidi]] wengine. Ingawa miguu yake ni mifupi, kutokana na nyayo zake kubwa zenye vidole vitano humwezesha asonge kwa rahisi kwenye theluji yenye kina.
 
Wolverini mzima ana ukubwa wa mbwa wa kawaida, urefu kwa kawaida kuanzia 65 hadi 107cm, mkia wa 17-26cm, na uzito wa 9-25kg, ingawa madume wakubwa waweza kuwa na uzito hadi 32kg. Madume wana ukubwa ulio wa 30% kubwa zaidi kuliko wa wajike. Wao ni mustelidi wakubwa zaidi wa kiardhi kati ya wote; [[ota-bahari]] na [[ota mkubwa]] wa Amazoni wazidi ukubwa wa wolverini.
 
Wolverini huwa na manyoya meusi na mazito ambayo ni ya haidrofobiki ambayo humpa upinzani kwa jalidi. Kwa sababu hii, wawindaji na wategaji walipenda kuwawinda ili kutumia manyoya yao na kutengeneza [[jaketi]] na [[parka]] dhidi ya hali ya hewa ya Aktiki. Wolverini wengine huwa na maskhara ya fedha na mstari wa manjano iliyokwajuka kutoka kwenye bega hadi mkia wenye manyoya mengi.
 
Kama mustelidi wengine, wao huwa na [[tezi la mkundu la manukato|matezi ya mkundu ya manukato]] ambayo hutumika. Kwa sababu ya manukato yao mabaya amepewa majina ya utani “dubu-kicheche” na “paka mbaya”
 
== Mwenendo ==
Wolverini huwa mwindaji mtendaji mwenye nguvu. Wolverini anajulikana kuua mawindo, kama vile: [[kulungu (Cervidae)|kulungu]], [[nungunungu]], [[kindi]], [[biva]], [[panyabuku]], [[sungura]], [[buku]], [[kipanya|vipanya]], [[sange]], [[kulungu aktiki]], [[kulungu mzungu|kulungu wazungu]], [[kulungu mkia-mweupe]], [[kulungu-baghala]], [[kondoo]], [[Alces alces|muusi]] na [[Cervus canadensis|elki]]. Wao pia wawinda [[konje]], [[minki]], [[mbweha]], [[linksi wa Kanada]], [[cheche]], [[linksi wa Ulaya]], [[koyote]] na vitoto wa [[mbwa-mwitu]].
 
== Jina ==
Wolverini hujulikana kama walafi wasiotosheka (kutoka jenasi ya Kilatini ya ''Gulo''). Jina la mnyama huyu kwa [[Kiswidi cha Kale]], ''fjellfräs'' linalomaanisha “paka wa milima” liliingia lugha ya Kijerumani kama ''Vielfrass'', linalomaanisha "mla nyingi". Jina lake kwa lugha nyingine za [[Kijerumani cha Magharibi]] hufanana na [[Kiholanzi]] ''veelvraat''.
 
Jina lake la [[Kifini]] ni ''ahma'' linalotoka ahmatti ambalo humaanisha "mlafi". Na pia kwa [[Kiestonia]] jina lake ni ''ahm'' lililo sawa na jina la [[Kifini]]. Kwa [[Kilithwania]] ni ''ernis'', kwa [[Kilatvia]] – ''tinis'' au ''āmrija''.
 
Lugha za [[Kislaviki cha Mashariki]] росомаха (''rosomaha'') na jina la [[Kipoli]] na [[Kicheki]] linatoka [[Kifini]] ''rasva-maha'' (tumbo nene). Na jina lake la [[Kihungaria]] ni ''rozsomák'' au ''torkosborz'' linalomaanisha "melesi-mlafi".
 
Katika sehemu za Kanada ambapo [[Kifaransa]] kinazungumzwa, wolverini anaitwa ''carcajou'' (karkajuu) kutoka lugha ya [[Kimontagnais]] ''kuàkuàtsheu''. Hata hivyo, katika [[Faransa]], jina la wolverini ni ''glouton'' (mlafi).
 
Neno la [[Kiingereza]] ''wolverine'' labda limaanisha "mbwa-mwitu mdogo". Jina lake kwa [[Kiproto-Norsi]] ''erafaz'' na [[Kinorsi cha Kale]] ''jarfr'' linapatikana lugha ya [[Kiisilandi]] kama ''jarfi'', [[Kinorwe]] ''jerv'', [[Kiswidi]] ''järv'' na [[Kideni]] ''jærv''.
 
 
 
[[Picha:Gulo_gulo_distribution.svg|thumb|left|Ramani inaonyesha maeneo yaliyokaliwa na wolverini (nyekundu)]]
 
[[Jamii:Wanyama]]