Western : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
d masahihisho ya lugha
Mstari 1:
'''Western''' (kutoka [[kiing.]] "West" - ''magharibi'') ni aina ya filamu yenye asili katika [[Marekani]]. Western husimulia hadithi za watu walioishi wakati wa [[karne ya 19]] hadi mwanzo wa [[karne ya 20]] Marekani ilipoenea katika sehemu za magharibi ya [[Amerika ya Kaskazini]]. Filamu kuhusu kipindi hiki zhilianzazilianza kupatikana tangu mwanzo wa karne ya 20.
 
Kazi muhimu ya filamu hizi ilikuwa kuwapa watu wa Marekani picha kuhusu historia yao na kuhusu tabia nzuri ya mababu walioanzisha na kueneza taifa yaolao. Ukweli wa kihistoria jinsi ilivyo katika hadithi za kitaifa ilibaki nyuma mara nyingi.
 
Filamu za Western zilitengenezwa baadayabaadaye pia huko [[Ulaya]] kama aina yahasa [[Spaghetti Western]] na mara nyingi zilicheza na aina za wahusika jinsizilivyokuwajinsi zilivyokuwa kawaida katika filamu za Marekani.
 
==Mazingira ya kihistoria ya filamu hizi==
Katika nyakati zile Marekani ilitawala tu sehemu za mashariki za Amerika ya Kaskazini tu na kupanua polepole kuelekea magharibi hadi kufikia [[Pasifiki]] na baadaye pia kutawala maeneo ya katikati. Palikuwa na eneo la "mpakani" (''frontier'') ambako wakulima walowezi na wafugaji kutoka Marekani waliingia katika nchi ya wakazi asilia au [[Maindio]] na kuanzisha makazi yao huko. Mashamba na miji yale yalikuwa nje ya eneo la Marekani yenyewe. Kwa hiyo maisha yalikuwa kwa muda bila sheria wala serikali. Hata kama maeneo mapya yaliingizwa katika [[Maungano ya Madola ya Amerika]] taasisi za serikali zilikuwa mbali kwa muda na kazi ya kuratibu maisha ilibaki mkononomkononi wa watu wenyewe katika eneo fulani.
 
[[Image:Buffalo Bill's Wild West Show.jpg|thumb|300px|Macowboy kazini]]
==Wahusika katika hadithi za Western==
Hadithi zinazosimuliwa katika filamu za western mara nyingi huwa na watu wafuatao:
* '''Cowboy''' au mchunga ng'ombe - anayeonyeshwa mara nyingi kama mtu mwenye kazi ngumu asiye na elimu lakini ni hodari. Kwa kawaida ni mtu mwema.
* '''Sheriff''' au mpolisi - anayepigana na waovu; huishi na kulala ofisini mwake anapoangalia pia wafungwa. Kazi yake ni piapamoja na kutetea wafungwa wale kama watu wa mji wanataka kuwanyonga mara moja. Kwa kawaida ana uwezo wa kutumia bunduki yake haraka sana. Huwa ni mtu mwema.
* '''Rancher''' au mwenye shamba la mifugo - yeye ni mwajiri wa macowboy. Ama ni mtajiri sana au yeye ni maskini anayeanza kujenga maisha yake na kupambana na matatizo ya kila aina. Mara nyingi ni mtu mwema lakini hutokea pia kama mbaya anayetaka kujitajirisha hata akimwua jirani
* '''Watu wa mjini''' - ama mwenye duka au mwenye kilabu. Anahofia waovu wanaopita mjini na kupora pesa zake. Kwa kawaida huwa mwoga asiye tayari kumsaidia sheriff.