Dwight D. Eisenhower : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d r2.7.3) (Roboti: Imeongeza jv:Dwight D. Eisenhower
d Minor fix using AWB
Mstari 1:
[[Picha:Dwight_D._Eisenhower,_official_Presidential_portrait.jpg|thumb|300px|Eisenhower kama Rais wa Marekani]]
'''Dwight David Eisenhower''' ([[14 Oktoba]], [[1890]] – [[28 Machi]], [[1969]]) alikuwa mwanajeshi na mwanasiasa kutoka nchi ya [[Marekani]]. Watu wengi walikuwa humwita '''Ike''' (tamka Aik). Wakati wa [[Vita Kuu ya Pili ya Dunia]] alikuwa jenerali mkuu aliyeongoza [[uvamizi wa Normandy]] tarehe [[5 Juni]], [[1944]]. Kuanzia mwaka wa [[1953]] hadi [[1961]] alikuwa Rais wa 34 wa Marekani. Kaimu Rais wake alikuwa [[Richard Nixon]].
 
== Maisha ==
Dwight Eisenhower alizaliwa tarehe 14 Oktoba, mwaka wa 1890, kama mtoto wa tatu wa David na Ida Eisenhower katika mji wa Denison, [[Texas]]. Watoto wote saba walikuwa wavulana, majina yao: Arthur, Edgar, Dwight, Roy, Paul (aliyefariki utotoni na [[dondakoo]]), Earl, na Milton. Kabla Dwight hajafikisha umri wa mwaka mmoja, wazazi wake walihamia mji wa Abilene, [[Kansas]], ambapo alilelewa na kuhitimu shule. Baada ya kufanya kazi mbalimbali za mikono, alifaulu mtihani wa kuingia chuo cha kijeshi cha [[Westpoint]] ambapo alihitimu mwaka wa [[1915]].
 
Tarehe [[1 Julai]], [[1916]], alifunga ndoa na Mamie Geneva Doud. Mtoto wao wa kwanza alizaliwa tarehe [[23 Septemba]], [[1917]], jina lake Doud Dwight Eisenhower lakini aliitwa ''Icky'' na wote. Alifariki na [[homa ya vipele vyekundu]] tarehe [[2 Januari]], [[1921]], akiwa na miaka mitatu tu. Mtoto wa pili, John Sheldon Eisenhower, alizaliwa mwaka wa [[1922]].
 
Eisenhower alihamishwa kikazi mahali mbalimbali siyo Marekani tu lakini pia nje, k.m. [[Panama]] na [[Ufaransa]]. Mara nyingi alifanya kazi ya ofisi ingawa alipendelea kazi ya kijeshi yenyewe. Nafasi yake alifika wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Kuanzia mwaka wa [[1942]], Eisenhower alikuwa kamanda, kwanza upande wa Afrika Kaskazini, akiwa na makao makuu mjini [[Algiers]], halafu aliongoza uvamizi wa [[Italia]], na mwishoni alitayarisha uvamizi wa Normandy tarehe 5 Juni, 1944.
 
Baada ya vita alikuwa kamanda mkuu wa [[NATO]]. Watu wengi wa [[Chama cha Republican]] walimpendelea agombee urais mwaka wa 1952, yeye lakini hakutaka kuingia mambo ya siasa. Hata hivyo aliandikishwa na kuwa mgombea wa Repulican. Baada ya kumshinda [[Adlai Stevenson III]], Eisenhower alikuwa Rais wa Marekani kwa awamo mbili hadi 1961. Wakati wa urais wake, [[vita ya Korea]] ilikomeshwa. Pia, siasa ya Marekani iliathiriwa na mawazo dhidi ya [[Wakomunisti]] yaliyotekelezwa na [[Joseph McCarthy]].
 
Baada ya kustaafu, Eisenhower alikaa pamoja na mke wake katika mji wa Gettysburg, [[Pennsylvania]]. Tarehe 28 Machi, 1969, alifariki hospitalini baada ya kupatwa na [[shtuko la moyo]].
 
== Marejeo ==