Bahari ya Karibi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d r2.7.2) (Roboti: Imeongeza pa:ਕੈਰੇਬੀਆਈ ਸਾਗਰ
d Minor fix using AWB
Mstari 2:
'''Bahari ya Karibi''' ni bahari ya pembeni ya [[Atlantiki]] iliyoko kusini ya [[Ghuba ya Meksiko]]. Upande wa magharibi imepakana na Amerika ya Kati, kusini na Amerika ya Kusini. Pinde la [[Visiwa vya Karibi]] linaitenga na Atlantiki yenyewe.
 
Bahari ya Karibi ina eneo la 2,754,000 km². Inafunika sehemu kubwa ya [[bamba la Karibi]]. Kina kikubwa kipo katika mfereji wa Kayman kati ya visiwa vya [[Kuba]] na [[Jamaika]] mwenye urefu wa 7,686 m chini ya [[UB]].
 
Kuna hori za bahari na ghuba mbalimbali kama ghuba ya Venezuela na ghuba ya Honduras.
 
== Ekolojia ==
Bahari hii inajulikana kwa [[mwamba wa tumbawe|miamba yake ya tumbawe]] ambayo ni mazingira ya aina nyingi za mimea, samaki na kasa. Miamba ya tumbawe ni msingi wa uvuvi na zinavuta watalii wengi.
 
Katika miaka ya nyuma tumbawe ziko hatarini kutokana na kupanda kwa halijoto ya maji. Tayari sehemu za tumbawe zimekufa. Mapatano ya nchi za Karibi yanatafuta njia za kuhifadhi mazingira haya ya pekee.
 
== Hali ya hewa ==
Kupanda kwa halijoto ya maji kumesababisha kuongezeka kwa dhoruba za [[tufani]] kali. Majira yake ni Juni na DisembaDesemba hasa wakati wa Agosti na Septemba. Kwa wastani kuna dhoruba kali 9 kila mwaka na 5 kati yao hufikia kiwango cha tufani. Dhoruba kali huanzia katika sehemu ya mashariki ya bahari ya Karibi kutokana na shindikizo duni la hewa. Dhoruba hizi huelekea mara nyingi upande wa magharibi-kaskazini lakini hugeuza kuelekea mashariki wakati wa kufikia maeneo yenye halijoto ya chini zaidi.
 
Tufani zinaleta uharibifu mwingi zikipita kwenye visiwa na makao ya watu lakini huharibu pia miamna ya tufani kutokana na kutupa kiasi kikubwa cha machanga na matope kwenye miamba hii.
 
== Historia ==
Jina la Karibi limetokana na makabila ya Wakaribi wenyeji waliokalia visiwa nya [[Antili Ndogo]] (kati ya kisiwa cha [[Puerto Rico]] na pwani la [[Venezuela]]) wakati wa kufika kwa [[Kristoforo Kolumbus]] mnamo mwaka 1500. Visiwa vikubwa vilikaliwa na wenyeji [[Waarawaki]] Wenyeji hawa walipotea kabisa kutokana na magonjwa yaliyoletwa na Wazungu Wahispania na vita dhidi ya wakoloni hawa.
 
Wahispania hawakuona umuhimu sana kutawala visiwa vyote vidogo hivyo Wazungu wengine walifuata na kuvamia visiwa mbalimbali. Waingereza, Wafaransa, Waholanzi na Wadenmark walishika visiwa mbalimbali na kuvifanya koloni zao.
Mstari 27:
Visiwa vingi vya Karibi vimepata uhuru katika karne ya 20. Athira ya Amerika ni kubwa siku hizi.
 
{{mbeguMbegu-jio-Karibi}}
 
[[Jamii:Bahari]]