Tofauti kati ya marekesbisho "Bessie Head"

11 bytes removed ,  miaka 8 iliyopita
Minor fix using AWB
(Minor fix using AWB)
[[Picha:Bessie head.jpg|thumb|right|250px]]
 
'''Bessie Emery Head''' ([[6 Julai]], [[1937]] - [[17 Aprili]], [[1986]]) hutazamwa kama mwandishi muhimu zaidi wa nchi ya [[Botswana]]. Alizaliwa katika eneo la [[Pietermaritzburg]], [[Afrika Kusini]], mwana wa mwanamke tajiri mweupe wa Afrika Kusini na mtumishi mweusi wakati ambapo uhusiano kati ya watu wa rangi tofauti ulikuwa kinyume cha sheria. Mamake alikuwa na ugonjwa wa kiakili; matukio yenyewe si hakika lakini kutokana na taarifa chache za Bessie Head, ambazo hudokezwa kana kwamba zimetoka katika kitabu alichoandika kuhusu maisha yake, mara nyingi huwa zimetungwa.
 
==Maisha ya kitaaluma==
Alikuwa mwalimu, halafu mwanahabari wa jarida la ''Drum'' katika miaka ya 1950 na '60.
 
==Kuhamia Botswana ==
Kazi yake mingi ya uandishi ilifanyika alipokuwa uhamishoni nchini Boswana, isipokuwa riwaya yake ya mapema ya ''The Cardinals'' (Makasisi) (iliyochapishwa baada ya kifo chake), iliyoandsikwa kabla ya yeye kuhamia Afrika Kusini.
 
Kwa njia Fulani, Bessie Head alibaki akiwa ametengwa katika nchi aliyohamia, na kuna watu wanaotazama kana kwamba aliipenda na kuichukia nchi hiyo kwa wakati mmoja. Wakati mwingine aliathirika na shida za kiakili na wakati mmoja aliweka tangazo hatharani akitangaza madai ya kutisha kuhusu aliyekuwa rais [[Seretse Khama]], ambayo ilimfanya akae kwa kipindi kifupi katika Hospitali ya Watu Wenye Ugonjwa wa Kiakili ya Lobatse. ''A Question of Power'' (Swali la Nguvu) ina msingi wake katika baadhi ya matukio haya.
 
==Kifo ==
Kifo chake mnamo mwaka wa 1986 (akiwa na umri wa miaka 49) kutokana na ugonjwa wa maini kilifanyika wakati alipokuwa ameanza kupata umaarufu na alipokuwa ameanza kuaga maisha ya umaskini.
 
==Ya ziada ==
 
Mnamo mwezi Julai mwaka wa 2007 makataba katika mji wa Pietermaritzburg yalipewa jina la Maktaba ya Bessie Head ili kumkumbuka.
 
* ''When Rain Clouds Gather'' (Wakati Mawingu ya Mvua Yanapokusanyika) (1968)
* ''Maru'' (1971)
* ''A Question of Power'' (Swali la Nguvu) (1974)
* ''Looking for a Rain God'' (Kumtafuta Mungu wa Mvua) (1977)
* ''The Collector of Treasures and Other Botswana Village Tales'' (Mkusanyaji wa Vitu vya Thamani na Hadithi Zingine za Vijiji vywa Botswana) (1977)
* ''A Bewitched Crossroad'' (Barabara yenye Njia Mbili iliyorogwa) (1984)
* ''A Woman Alone: Autobiographical Writings'' (Mwanamke Peke Yake: Maadiko Kuhusu Maisha Yake) (1990)
* ''A Gesture of Belonging: Letters from Bessie Head, 1965-1979'' (Ishara ya Kuwa na Makao:Barua kutoka Bessie Head) (1991)
* ''The Cardinals'' (Makasisi) (1993)
 
==Tuzo ==
 
* 2003 - ''Tuzo la Dhahabu la Ikhamanga'' kwa '' mchango wake wa kujitolea kuendeleza fasihi na mchango wa mabadiliko ya kijamii, uhuru na amani.''<ref name='Award'>{{cite news | first= | last= | coauthors= | title=Profile of Bessie Head | date= | publisher=S A National Orders | url =http://www.thepresidency.gov.za/orders_list.asp?show=172 | work = | pages = | accessdate = 2007-04-26 | language = }}</ref>
 
 
==Citation==
{{Marejeo}}
<references/>
 
==External links==
* [http://www.bessiehead.org Bessie Head Heritage]
* [http://www.englishdaily626.com/stories.php?017 Looking for rain God - A short story]
 
{{DEFAULTSORT:Head, Bessie}}
9,497

edits