Tofauti kati ya marekesbisho "Dk. Omar Ali Juma"

3 bytes removed ,  miaka 8 iliyopita
Minor fix using AWB
d (r2.7.3) (Roboti: Imeongeza no:Omar Ali Juma)
(Minor fix using AWB)
'''Dk. Omar Ali Juma''' ([[26 Juni]], [[1941]] – [[4 Julai]], [[2001]]) alikuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu nchini [[Tanzania]], iliyokuwa inaongozwa na Rais [[Benjamin William Mkapa]].
 
==Wasifu==
===Maisha ya awali===
Dk. Omar alizaliwa tarehe [[26 Juni]], [[1941]] katika kijiji cha Wawi, Wilaya ya Chakechake, Kusini mwa Mkoa wa Pemba.
 
Elimu yake ya msingi aliipata katika Shule ya Msingi ya wavulana ya Chake, ambayo kwa sasa inajulikana kama Shule ya Msingi Michakaini tangu mwaka [[1949]] mpaka mwaka [[1957]].
 
Dk. Omar aliendelea na masomo yake na mwaka [[1982]] alikuwa mmoja wa wahitimu katika Chuo Kikuu cha Reading, [[Uingereza]] na pia kiongozi huyu alipata fursa ya kwenda kusoma katika Chuo cha Kivukoni Ideological mwaka [[1982]].
 
==Shughili za Kiserikali==
Dk. Omar Ali Juma alikuwa mfanyakazi wa Serikali ya Mapinduzi ya [[Zanzibar]] tangu mwaka [[1967]] hadi mwaka [[1984]] ambapo alihamishiwa katika Serikali ya [[Jamhuri ya Muungano wa Tanzania]] mwaka [[1995]] hadi alipofariki dunia.
Mwaka 1971 -1972 alikuwa Ofisa Mifugo, pia alikuwa Ofisa Mkuu wa Mifugo katika miaka ya 1972-1978.
 
Wakati mwaka 1978-1984, alifanikiwa kushika wadhifa wa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mifugo, mwaka 1984-1987 alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo, Zanzibar, na Januari 1988 - 1995, alikuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
 
==Viungo vya Nje==
9,527

edits