Tofauti kati ya marekesbisho "Emin Pasha"

2 bytes removed ,  miaka 7 iliyopita
Minor fix using AWB
d (r2.7.2) (roboti Nyongeza: eu:Emin Paxa)
(Minor fix using AWB)
[[Picha:Eminpasha.jpg|right|thumb|Eduard Schnitzer aliyejulikana kama ''Emin Pasha'']]
'''Mehmet Emin Pasha''' ([[28 Machi]], [[1840]] - [[23 Oktoba]], [[1892]]) alikuwa daktari, mtaalamu na gavana wa jimbo la [[Ekwatoria]] la nchi ya [[Misri]]. Kwa asili alikuwa [[Ujerumani|Mjerumani]] lakini alifanya kazi hasa katika [[Milki ya Osmani]].
 
== Wasifu ==
Emin Pasha alizaliwa kwa jina la '''Isaak Eduard Schnitzer''' mjini [[Opole]] (leo iko nchini [[Poland]]), wazazi wake wakiwa [[Wayahudi]]. Baada ya kifo cha baba mwaka wa 1845, mama aliolewa tena na kubatizwa pamoja na watoto wake kuwa [[Ukristo|Wakristo]]. Alihitimu chuo kikuu cha [[Berlin]] katika somo la [[tiba]] mwaka wa 1864 na kuondoka moja kwa moja kusafiri mji wa [[Konstantinopoli]] ili kufanya kazi chini ya [[Milki ya Osmani]]. Kuanzia mwaka wa 1875 alitumia jina la '''Mehmet Amin'''; wakati huo aliishi mjini [[Khartoum]] (leo iko nchini [[Sudani]]). Mwaka wa 1878 alimfuata [[Charles George Gordon]] kuwa gavana wa jimbo la Ekwatoria. Tangu mwaka wa 1881 alilazimishwa kujitegemea katika jimbo lake kwa sababu ya uasi wa [[Muhammad Ahmad]]. Mwaka wa 1886 alipewa cheo cha ''Pasha''. Mwaka wa 1888, Emin Pasha alikombolewa na [[Henry Morton Stanley]], nao pamoja wakaanza safari ya kwenda [[Bagamoyo]] ambapo walifika mwaka wa 1890. Emin Pasha aliuawa na Waarabu wawili wakati alipochunguza maziwa ya Afrika Mashariki.
 
{{mbeguMbegu-mtu}}
 
{{BD|1840|1892|Emin Pasha}}
{{commonsCommons|Emin Pasha}}
 
[[Jamii:Wataalamu wa Ujerumani]]
9,497

edits