Ibn Battuta : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d r2.7.3) (Roboti: Imeongeza ba:Ибн Баттута
Minor fix using AWB
Mstari 2:
'''Abu Abdullah Muhammad Ibn Battuta''' ([[Kar.]]: أبو عبد الله محمد بن بطوطة) alikuwa msafiri, mpelelezi na mtaalamu Mwarabu wa [[karne ya 14]]. Kwa usafiri mgumu wa siku zile alitembelea nchi na kuvuka umbali mkubwa kushinda mtu yeyote wa siku zile anayejulikana. Kutoka kwake tunayo taarifa ya kwanza kuhusu mji wa [[Kilwa Kisiwani]].
 
Alizaliwa tarehe [[24 Februari]], [[1304]] mjini [[Tanger]] ([[Moroko]]). Mwaka 1325 alihiji kwenda [[Makka]] na baada ya [[hajj]] hakurudi bali aliendelea kusafiri. Alitembelea karibu nchi zote zilizokaliwa na Waislamu. Kwa jumla alisafiri kwa miaka 30 akivuka umbali wa karibu km 120,000 (hii ni kama kuzunguka dunia yote mara tatu).
 
Habari zake zimepatikana katika taarifa yake aliyoiandika mwenyewe.
 
Katika safari yake ya kwanza alikwenda [[Makka]] kupitia [[Misri]], [[Yerusalemu]] na [[Dameski]]. Baada ya kumaliza [[hajj]] akajiunga na msafara kwenda [[Baghdad]] akaona ufalme wa [[Khan wa Il]] na kutembelea [[Uajemi]]kabla ya kurudi Moroko.
 
Safari yake ya pili ilianza tena kama hajj na safari hii akaendelea kuangalia maeneo ya [[Bahari ya Shamu]] na pwani ya [[Afrika ya Mashariki]]. Akafika hadi [[Kilwa]]kisha akarudi Makka kupitia [[Omani]].
 
Baada ya kupumzika Makka alikata shauri kuona himaya ya Sultan wa [[Delhi]] ([[Uhindi]]).
Aliamua kujaribu njia kupita [[Uturuki]] kwa sababu alisikia ya kwamba palikuwa na misafara kati ya Waturuki [[Waseldjuki]] na Uhindi. Baada ya kuvuka [[Bahari Nyeusi]] alifika katika milki ya [[Kundi la Dhahabu]] akaendelea katika msafara wa [[Khan]] wa nchi. Alipofika mji mkuu [[Astrakhan]] aliombwa na Khan wa Kundi la Dhahabu mwenyewe kumsindikiza mke wake aliyetaka kutembela nduguye nyumbani kwake [[Konstantinopoli]]. Hivyo Ibn Battuta alifika mara ya kwanza katika nchi nje ya Waislamu.