Louis Armstrong : Tofauti kati ya masahihisho
Content deleted Content added
Xqbot (majadiliano | michango) d r2.7.3) (Roboti: Imeongeza pms:Louis Armstrong |
Minor fix using AWB |
||
Mstari 1:
[[Picha:Louis Armstrong restored.jpg|thumbnail|right|300px|Louis Armstrong]]
'''Louis Armstrong''' ([[4 Agosti]]
Louis alizaliwa katika jiji la [[New Orleans]], Louisiana, alipewa jina la utani "Satchel Mouth" ambalo baadaye lilikuja kukatishwa kama "Satchmo". Maisha ya Louis utotoni mwake yalikuwa ya shida kwani alitumia muda mwingi bila maana na vijana wa mjini New Orleans. Hii ilitokana na baba yake William Armstrong kuitelekeza familia, hiyo ilimfanya Louis kuishi bila kuwa na baba. Hivyo alilelewa na mama yake Mary Albert Armstrong (1886-1942). Baada ya kufariki Mary, Louis na mdogo wake wa kike aliyeitwa Betrice Armstrong Collins (1903-1987) wakiwa chini ya uangalizi wa bibi yao Josephine, Louis kwanza alianza kujifunza kupiga koneti (hii ni aina ya tarumbeta dogo).
Ilikuwa ni tarumbeta yake ya kwanza kuinunua na ilitokana na pesa zake za mkopo alizopata kutoka kwa akina Karnofsky (hii ni jamii ya wahamiaji wenye asili ya Kiyahudi na Kirusi). Louis alipenda kusikiliza wanamuziki wa kizamani kila alipopata nafasi, alijifunza kutoka kwa Bunk Johnson, Buddy Petit na yote kuhusu Joe "King" Oliver ambaye alikuwa kama mshauri wake na aliyempa uzoefu na zaidi alimjenga kijana Louis. Louis baadaye alihudhuria brasi bendi zinazotumbuiza kwenye meli za mto [[Mississippi]]. Kwanza alianza kutembea na benndi ya The Wellregarded band iliyokuwa ikivinjari kwa meli kwenye mto wa Mississipi hiyo ilimfanya kutumia muda wake vizuri kama aliyekwenda chuo kikuu, na tangu hapo ilimpa uwezo na uzoefu wa kufanya kazi kwa kuziandika na kupanga mipango ya kazi zake, wakati Oliver alipoondoka New Oleans 1919, Louis alichukua nafasi yake kwenye bendi ya Kid Ory's band, hii ilikuwa ni bendi iliyokuwa kali na ya kiwango cha juu mjini hapo.
{{Commons category}}
{{
{{DEFAULTSORT:Armstrong, Louis}}
|