NASA : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d Roboti: Imeongeza pnb:ناسا
Minor fix using AWB
Mstari 1:
'''NASA''' ni kifupi cha [[Kiingereza]] cha "'''National Aeronautics and Space Administration'''" (Mamlaka ya Marekani ya Usafiri wa Anga). Mamlaka hii ilianzishwa 1958. Wajibu wake ni kusimamia miradi ya serikali ya [[Marekani]] ya kuendesha utafiti na uchunguzi wa anga. NASA inatawala utengenezaji wa roketi za kurusha vyombo vya angani na vyombo vya angani vyenyewe.
 
[[Picha:Mercury 3.jpg|thumb|200px|right|Roketi iliyorusha "Freedom 7" na Alan Shepard Jr.angani tar. 5.5.1961]]
 
Miradi ya NASA ilianzishwa kutokana na [[Mshtuko wa Sputnik]] yaani baada ya [[Warusi]] kushtusha dunia kwa kupeleka vyombo vya angani vya kwanza katika mradi wao wa [[Sputnik]]. Ulifuatwa na mradi wa "[[Vostok]]" ambao tarehe [[12 Aprili]], [[1961]] ulimfikisha [[Yuri Gagarin]] angani akiwa mtu wa kwanza huko kwenda angani.
 
Mradi wa kwanza wa NASA ulikuwa [[Mradi wa Mercury]] uliotakiwa kuonyesha ya kwamba wanaanga wanaweza kukaa angani kwa muda fulani. Alan B. Shepard Jr. alikuwa Mmarekani wa kwanza angani kwa muda wa dakika 15; John Glenn alikuwa Mmarekani wa kwanza wa kuzunguka dunia tarehe [[20 Februari]], [[1962]] kwa chombo cha angani "Friendship 7".
 
Mradi huo ulifuatwa na [[Mradi wa Gemini]] kuanzia mwaka 1965 ulionyesha ya kwamba watu wanaweza kukaa angani kwa muda wa siku kadhaa hata kutekeleza shughuli fulani. Gemini iliandaa [[Mradi wa Apollo]] uliopeleka watu wa kwanza [[mwezi]]. Chombo cha angani "Apollo 11" kilifikisha wanaanga [[Neil Armstrong]] na [[Buzz Aldrin]] kwenye uso wa mwezi tarehe [[20 Julai]], [[1969]] na kuwarudisha dunia tena.
 
Kutoka mwanzo ule kuna miradi mingi iliyofuata.