Nikolaus von Zinzendorf : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
→‎Maisha: Minor fix using AWB
Mstari 3:
 
==Maisha==
Alizaliwa mjini [[Dresden]] katika [[familia]] ya makabaila Wajerumani [[Walutheri]]. Baba yake alikufa alipokuwa mdogo, akalelewa na bibi yake aliyemshawishi kwa mwelekeo wa [[uamsho]] wa Kikristo wa [[upietisti]].
 
Baada ya kumaliza [[shule]] alisoma [[sheria]] kwenye [[chuo kikuu]] cha [[Wittenberg]]; baada ya masomo yake alifanya safari ya kuzunguka [[Ulaya]], jinsi ilivyokuwa kawaida kwa vijana makabaila wa siku zile. Kwenye safari hii alikutana na kuwa rafiki na viongozi wa [[madhehebu]] mbalimbali kama [[Wareformed]], [[Wakatoliki]], Walutheri na wengine.
 
Kati ya miaka [[1721]] na [[1732]] alikuwa mshauri wa kisheria kwenye [[ikulu]] ya [[mfalme]] [[August II (Polonia)|August wa Saksonia]] huko Dresden.
Mstari 11:
[[picha:Graf Nikolaus Ludwig von Zinzendorf Denkmal Herrnhut.jpg|thumb|[[Sanamu]] ya kumbukumbu ya Zinzendorf huko Herrnhut]]
 
Mwaka [[1722]] alimwoa Erdmuthe na mwaka uleule alinunua mashamba ya kikabaila ya [[Berthelsdorf]] kutoka bibi yake. Ilikuwa eneo dogo lenye [[kijiji]] kimoja alipotawala kama [[mtemi]] chini ya [[Kaisari]] pekee, ingawa eneo lake dogo lilikuwa ndani ya [[jimbo]] kubwa La [[Saksonia]].
 
Katika eneo hili alianza kupokea wakimbizi kutoka [[Moravia]] waliokuwa wafuasi wa [[Umoja wa Ndugu]] wa kale, mwelekeo wa Kiprotestanti wa [[Bohemia]] na Moravia uliopigwa marufuku tangu mwisho wa [[vita ya miaka 30]]. Aliwapa wakimbizi hao ardhi walipojenga kijiji kipya cha [[Herrnhut]]; hapa waliunda "Umoja wa Ndugu ulioanzishwa upya" unaojulikana kama [[Kanisa la Moravian]] au pia Ndugu wa Herrnhut.
 
Kutoka Herrnhut desturi ya kuchagua [[ubeti]] wa [[Biblia]] kama neno la mwongozo kwa kila siku ilianza kusambaa: mkusanyo wa maneno haya yanajulikana kama [[Kiongozi Kalenda]].
 
Mwaka [[1731]] Zinzendorf alitembelewa na nduguye mkabaila mmoja kutoka [[Denmark]] aliyefika pamoja na mtumishi wake Mwafrika kutoka [[Visiwa vya Karibi]] aliyewahi kuwa [[mtumwa]]. Masimulizi ya huyu Mwafrika yalihamasisha ndugu wa Herrnhut kutuma wahubiri kwenda Karibi na hii ilikuwa chanzo cha uenezaji wa kimataifa wa kanisa la Moravian.
 
Zinzendorf aliwaandalia safari akitumia mawasiliano na ikulu ya mfalme wa Denmark. Zinzendorf mwenyewe alitembelea ndugu wa Herrnhut waliosafiri kuhubiri [[Saint Thomas (Karibi)]], [[Marekani]], [[London]] na nchi jirani za [[Bahari Baltiki]].
 
Aliendelea kusoma [[teolojia]] na mwaka [[1734]] akabarikiwa kama [[mchungaji]] Mlutheri. Hata hivyo alifukuzwa katika Saksonia (hapa Ulutheri ulikuwa [[dini rasmi]]) kutokana na shaka kuhusu [[imani]] yake, akapaswa kuhamia sehemu nyingine za Ujerumani alipoanzisha jumuiya mpya ya wafuasi wa Umoja wa Ndugu.
 
Mwaka [[1737]] alibarikiwa kama askofu wa Umoja wa Ndugu na askofu wa Umoja huu kutoka [[Polandi]] ambako shirika chache za Umoja wa kale ziliweza kuendelea.
 
Mwaka [[1747]] aliruhusiwa kurudi Saksonia na ndugu wa Herrnhut walikubaliwa kama jumuiya iliyoshikamana na kanisa la Kilutheri la Saksonia. [[Mke]] wake Erdmute aliyezaa watoto 12 aliaga dunia mwaka [[1756]], hivyo baadaye akamwoa [[Anna Nitschmann]] mmoja wa wakimbizi kutoka Moravia.
 
Zinzendorf anakumbukwa kama baba wa kiroho wa kanisa la Moravian. Alitunga nyimbo nyingi zinazoimbwa kwa Kijerumani hadi leo na nyingine zimetafsiriwa katika [[lugha]] mbalimbali.