Njiamzingo : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'File:Orbital motion.gif|thumb|200px|Obiti ya gimba dogo (kama satelaiti) linalozunguka gimba kubwa (kama dunia); <br>kani ya velositi inataka kulipeleka mbele...'
 
No edit summary
Mstari 5:
==Uwiano wa kani katika obiti==
Fizikia ya obiti inatazama kani au nguvu mbili. Ya kwanza ni [[velositi]] ya gimba dogo inayoelekea kwenda mbele mbali na mahali pake. Ya pili ni [[graviti]] inayovuta gimba dogo kuelekea gimba kubwa. Obiti iko pale ambako hizi ngvu mbili zinalingana. Kama kani ya velositi ingekuwa kubwa zaidi gimba dogo lisingezunguka bali kutoka. Kama kani ya graviti ingekuwa kubwa zaidi gimba dogo linaanguka chini.
 
==Mfano wa "Mzinga wa Newton"==
Mwanafizikia Isaac Newton aliwaza mfano unaoeleza vizuri kani zinazoathiri obiti.
Aliwaza mfano wa [[mzinga]] unaosimamishwa juu ya mlima mrefu. Mzinga huu unaweza kurusha risasi kwa mwelekeo wa mlalo tena kwa kasi mbalimbali. Athira ya msuguano wa hewa dhidi ya risasi angeacha kando au kuwaza mlima mrefu kiasi cha kufikia juu ya angahewa ya dunia.
 
Kama mzinga unarusha risasi yake kwa velositi ndogo itaenda mbele kiasi halafu kuanguka chini (A). Kama kasi au velositi inaongezwa itaanguka mbali zaidi(B).
 
Wakati kasi inaongezeka zaidi kuna hali ambako risasi haianguki tena inazunguka dunia na kumailisha obiti ya duara (C).
 
Kama kasi inaongezeka tena obiti inachukua umbo la duaradufu. Mahali ambako obiti iko karibu na dunia ni mahali pa kufyatuliwa na 180 kinyume chake; katikati ni nukta ambako obiti iko mbali na dunia. (D)
 
Wakati kasi inaongezeka zaidi kuna risasi inafikia velositi ya kutoka katika graviti ya sayari (E).
 
Hali halisi makadirio ya makombora ya kurusha satelaiti na vyombo vya angani vinafuata maelezo hapo juu. Kama kombora linatikwa kubeba satelaiti kama vile satelaiti ya televisheni au ya mwawasiliano ni lazima kukadiria velositi ya kombora kulingana na uzito wake na mahali panapotakiwa kufikia angani na hivyo kupeleka satelaiti katika obiti aina ya (C) au (D).
 
Wakati chombo cha angani kitakiwa kupelekwa safari ya kwenda mwezi au sayari nyingine sharti kufikia "velositi ya kutoka" katika graviti ya dunia.
 
==Historia ya utafiti wa obiti==