Daudi (Biblia) : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Addbot (majadiliano | michango)
d Bot: Migrating 70 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q41370 (translate me)
Mstari 18:
Kadiri alivyozidi kupendwa na Mungu na watu, Sauli alimchukia kwa [[kijicho]] na kutaka kumuua (1Sam 18:6-16). Daudi alipolazimika kukimbia na kuunda kikosi chake akapata nafasi rahisi ya kumuua Sauli lakini alijizuia kwa kuheshimu [[krisma]] aliyopakwa awe mfalme (1Sam 24 na 26): hivyo ni mfano bora wa kujali [[wito]] wa Kimungu.
 
Baada ya kufanywa mfalme wa [[kabila]] lake ([[Kabila la Yuda|Yuda]], yaani Kusini) na ya kupigana [[vita]] na mwana wa [[marehemu]] Sauli, Daudi akakubaliwa kuwa mfalme wa Israeli yote (yaani Kaskazini pia): pamoja na taarifa hiyo, [[2Sam]] 5:1-12 inatuambia alivyoteka Yerusalemu uliokuwa bado mikononi mwa [[dini za jadi|Wapagani]] akaifanya makao makuu ya kisiasa na ya kidini ya taifa lote la Mungu ili aunganishe Kaskazini na Kusini katika mji huo uliopo katikati. Kuanzia hapo [[Yerusalemu]] ukawa mji mtakatifu wa [[dini]] tatu zinazomuabudu Mungu wa [[Abrahamu]].
 
2Sam 6 inasimulia [[sanduku la agano]] lilivyohamishiwa Yerusalemu kwa shangwe kubwa; hasa Daudi alicheza mbele ya Mungu kwa nguvu zake zote huku amevaa nguo ndogo ya kikuhani tu, bila ya kujijali kama mfalme.
 
Kwa [[unyenyekevu]] wake huo alimpendeza Mungu akapewa naye ahadi ya ajabu, yaani kwamba ufalme wake utadumu milele (2Sam 7). [[Utabiri]] huo wa [[nabii]] [[Nathani]] ukaja kuongoza [[tumaini]] la Waisraeli hasa walipodhulumiwa, k.mf. zamani za [[Yesu]] chini ya [[ukoloni]] wa Kirumi, ambapo wote walimtazamia [[mwana wa Daudi]] mwenye kurudisha ufalme wa Israeli.
 
Pamoja na hayo, kisha kupewa ahadi hiyo alikwenda mbele ya Mungu na kusali vizuri kama kawaida yake hata nje ya ibada: [[sala]] yake ya sifa na [[shukrani]] imejaa mshangao kwa ukuu wa Mungu na [[fadhili]] zake na kumalizika kwa ombi nyenyekevu.
Mstari 28:
Ingawa hakukubaliwa kumjengea Mungu [[hekalu]] la ajabu alivyokusudia, amekuwa mwalimu wa sala kwa nyakati zote: hata leo [[liturujia]] ya [[Uyahudi]] na ya [[Ukristo]] inategemea sana zaburi zake.
 
Matendo mengine tofauti yaliyoathiri sana maisha ya Daudi ni [[dhambi]] alizotenda kwa ajili ya mke wa [[Uria Mhiti]], yaani [[uzinifu]], [[unafiki]], [[ulevyaji]] na [[uuaji]] wa askari huyo mwadilifu (2Sam 11). Basi, [[nabii]] [[Nathani]] akamuendea ili kumlaumu na kumtabiria adhabu mbalimbali, hasa kwamba [[upanga]] hautaondoka nyumbani kwake (2Sam 12:1-25).
 
Ikawa hivyo hasa kwa sababu ya [[Absalomu]] mwanae ambaye alimuua kaka yake (2Sam 13:22-37) na baada ya kusamehewa akafanya [[njama]] hata akamfukuza Daudi toka Yerusalemu (2Sam 14:28-15:29) akazini na masuria wake mahali pa wazi (2Sam 16:20-23). Hata hivyo Daudi akazidi kumpenda na alipoambiwa ameuawa akamlilia kwa namna ambayo iliwashangaza na kuwachukiza waliompigania: lakini yeye ambaye alijiombea na kupewa [[msamaha]] wa Mungu hakumchukia mwanae aliyehatarisha maisha yake (2Sam 18:19-20:8).