ANC : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 10:
Umoja wa Vijana wa ANC (ANC Youth League) ulianzishwa 1944 na [[Nelson Mandela]], [[Walter Sisulu]] na [[Oliver Tambo]] ukaongeza ukali katika mwendo wa kupinga ubaguzi wa rangi bila kutumia mabavu au silaha. 1947 ANC iliamua kushikama kwa karibu na vyama vya Natal Indian Congress na Transvaal Indian Congress.
 
==Kipindi cha [[Apartheid]] (ubaguzi wa rangi wa kisheria)==
Ushindi wa National Party katika uchaguzi wa raia weupe pekee mwaka 1948 ulileta mwanzo wa siasa ya [[Apartheid]] iliyolenga kuwaondoa Waafrika kabisa katika siasa ya Afrika Kusini hata katika eneo lake isipokuwa kwa wafanyakazi waliotakiwa kukaa kwa muda tu na uhamisho wa Waafrika wote katika mikoa ya [[Bantustan]].
 
Kadiri jinsi ukandamizaji dhidi ya Waafrika ulivyoongezeka ANC ikaongeza ukali wa upinzani hadi kuunda kwa siri idara ya kijeshi kilichoitwa "Umkhonto We Sizwe" ("mkuki wa taifa") iliyoanzishwa na Nelson Mandela. Azimio la kuchukua hatua hii ilichukuliwa baada ya [[mauaji ya Sharpeville]] tar. [[21 Machi]] [[1960]].
Mstari 20:
Harakati ya wanafunzi Waafrika wa Afrika Kusini walioanza kupigana na polisi tangu 1976 imekua bila kuathiriwa sana na ANC. Upinzani huu uliendelea pamoja na migomo ya wafanyakazi kwenye migodi.
 
==Mwisho wa ubaguzi wa rangiApartheid==
Hadi mwisho wa miaka ya 1980 serikali ya Makaburu iliona ugumu kuendelea na siasa ya Apartheid jinsi ilivyokuwa. Gharama za ukandamizaji wa upinzani zilikua na pamoja na mwisho wa "[[vita baridi]]" siasa ya nchi zilizowahi kusaidia serikali ya Apartheid ikaanza kubadilika kwa kudai kuongeza haki za Waafrika.