Ali Hassan Mwinyi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
 
No edit summary
Mstari 1:
'''Ali Hassan Mwinyi''' amezaliwa tarehe 8, mwezi wa Mei, mwaka wa 1925, kwenye kisiwa cha [[Unguja]] (Zanzibar). Alikuwa Rais wa Pili wa Tanzania kuanzia 1985 hadi 1995. Aliyemtangulia ni Mwalimu [[Mwalimu Julius Nyerere]], na aliyemfuata ni [[Benjamin Mkapa]]. Kabla hajachaguliwa kuwa Rais, Mwinyi alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Makamu Rais. Pia alikuwa mwenyekiti wa [[Chama Cha Mapinduzi]] (CCM) kuanzia 1990 hadi 1996.
 
Wakati wa urais wa Mwinyi, sera za [[Ujamaa]] zilianza kugeuzwa. Badala yake sera za [[soko huru]] zilianzishwa, masharti ya kuingiza bidhaa kutoka nchi za nje yalipunguzwa na uanzishaji wa biashara ya watu binafsi ulihamasishwa. Mwaka wa 1991, uanzishaji wa vyama vingi uliruhusiwa.