Petro Claver : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Legobot (majadiliano | michango)
d Bot: Migrating 16 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q167458 (translate me)
Petro
Mstari 1:
[[Image:StPeterClaver.jpg|thumb|right|250px|Mt. Pedro Claver, mtume wa [[Wanegro]].]]
 
'''Petro Claver, [[S.J.]]''', ({{lang-es|San Pedro Claver Corberó}}) ([[Verdu]], [[Urgell]], [[Lleida]], [[Catalonia]], [[Hispania]], [[26 Juni]] [[1581]] – [[Cartagena, Colombia|Cartagena]], [[Kolombia]], [[8 Septemba]] [[1654]]) alikuwa [[padri]] [[Mjesuiti]] [[mmisionari]] huko [[Amerika Kusini]].
 
Kutokana na maisha yake aliyoyatoa kwa [[nadhiri]] ya kujifanya [[mtumwa]] wa watumwa, anaheshimiwa kama [[mtakatifu]] [[msimamizi]] wa [[misheni]] zote za [[Kanisa Katoliki]] kwa watu wenye asili ya [[Afrika]].
 
Katika miaka 40 ya kuhudumia [[Wanegro]] wa Kolombia kiroho na kimwili, inakadiriwa [[ubatizo|aliwabatiza]] 300,000 hivi.
 
[[Papa Pius IX]] alimtangaza [[mwenye heri]] tarehe [[16 Julai]] [[1851]], na [[Papa Leo XIII]] alimfanya [[mtakatifu]] tarehe [[15 Januari]] [[1888]].
 
==Maisha==
Petro Claver alizaliwa mwaka 1581 huko [[Verdu]] katika familia tajiri ya wakulima [[Wakatoliki]] sana<ref name=suau>[http://www.newadvent.org/cathen/11763a.htm Suau, Pierre. "St. Peter Claver." The Catholic Encyclopedia. Vol. 11. New York: Robert Appleton Company, 1911. 2 Apr. 2013]</ref>, miaka 70 baada ya [[Mfalme Ferdinando wa Hispania]] kuanzisha [[biashara ya watumwa]] kwa kuruhusu ununuzi wa Waafrika 250 huko [[Lisbon]] kwa ajili ya ma[[koloni]] yake ya [[Amerika]].
 
Katika [[karne ya 17]] biashara hiyo kutoka Afrika kwenda [[Amerika]] ilikuwa kubwa.<ref name=kopc>[http://www.kofpc.org/index.php?option=com_content&view=article&id=57&Itemid=54 "St. Peter Claver", Knights of Peter Claver]</ref>
 
Ni katika [[mazingira]] hayo kwamba Petro alijisikia kuongozwa na [[Mungu]] afanye kazi kwa juhudi zote.
 
Akiwa [[mwanafunzi]] wa [[Chuo kikuu]] cha [[Barcelona]],<ref name=suau/> Petro alijulikana kwa [[akili]] na [[moyo wa
 
Baada ya kusomea huko miaka miwili, aliandika hivi katika daftari lake dogo alilolitunza maisha yake yote: "Natakiwa kujitoa nimtumikie Mungu hadi kifo, nikijifananisha na mtumwa."
 
Baada ya kumaliza masomo yake, Petro alijiunga na [[Shirika la Yesu]] huko [[Tarragona]] akiwa na [[umri]] wa miaka 20. Kisha kumaliza [[unovisi]], alitumwa kusoma [[falsafa]] huko [[Palma, Mallorca]].
 
Akiwa huko alifahamiana na [[bawabu]] wa [[chuo]] cha shirika, Mt. [[Alfonso Rodriguez]], [[bradha]] maarufu kwa [[utakatifu]] na kwa [[karama]] ya [[unabii]]. Rodriguez alijisikia ameambiwa na Mungu kwamba Claver alitakiwa kutumia maisha yake katika makoloni ya [[Hispania Mpya]] barani Amerika, akamhimiza mara nyingi kuitikia wito huo.<ref name=suau/>
 
Claver alijitolea kwenda akatumwa katika [[ufalme]] wa [[Granada Mpya]], alipofikia katika [[bandari]] ya [[Cartagena, Colombia|Cartagena]] mwaka [[1610]].<ref name=foley>[http://www.americancatholic.org/Features/Saints/saint.aspx?id=1133 Foley OFM, Leonard. ''Saint of the day, Lives, Lessons, and Feast'', (revised by Pat McCloskey OFM), Franciscan Media, ISBN 978-0-86716-887-7]</ref>
 
Akitakiwa kusubiri miaka 6 kabla ya kupewa [[upadrisho]] wakati wa kusoma [[teolojia]], aliishi katika nyumba za Wajesuiti huko [[Tunja]] na [[Bogotá]]. Katika miaka hiyo ya maandalizi, aliguswa sana na ukali uliotumika dhidi ya watumwa, pamoja na hali yao ngumu kwa jumla.
 
Cartagena ilukuwa kituo cha [[biashara]] hiyo. Kwa mwaka watu 10,000 walikuwa wanashushwa bandarini kutoka [[Afrika Magharibi]] baada ya [[safari|kusafirishwa]] melini katika hali ya kutisha, kiasi kwamba inakadiriwa thuluthi moja walikuwa wanakia njiani. Ingawa biashara hiyo iliharamishwa na [[Papa Paulo III]] na [[Papa Urban VIII|Urban VIII]]<ref name=kopc/> faida yake kiuchumi ilifanya iendelee kustawi<ref name=foley/>
 
Mtangulizi wa Claver katika [[utume]] wake wa moja kwa moja, [[padri]] [[Alonso de Sandoval]], S.J., alimuandaa na kumuongoza hata kwa mfano wake.<ref name=foley/> Sandoval alimuona Claver kuwa mwanafunzi bora. Mwenyewe alikuwa amehudumia watumwa kwa miaka 40 kabla Claver hajafika kumpokea katika kazi hiyo. Sandoval alikuwa amejitahidi kujifunza [[desturi]], [[ibada]] na [[lugha]] za Waafrika, akafaulu kiasi cha kuweza kuandika [[kitabu]] juu ya hayo mwaka [[1627]] baada ya kurudi [[Seville]].
 
Petro alipoweka [[nadhiri za daima]] katika shirika mwaka [[1622]], alisaini hivi kwa [[Kilatini]] hati ya [[kujiweka wakfu]]: ''Petrus Claver, Aethiopum semper servus'' (yaani: Petro Claver, mtumwa wa kudumu wa Waafrika).
 
[[File:131 Cathedral San Pedro Claver Dome Cartagena.JPG|thumb|Kanisa la Mt. Petro Claver huko [[Cartagena, Colombia]], alipoishi na kufanya kazi.]]
Sandoval alikuwa akitembelea watumwa mahali pa kazi zao, kumbe Claver aliona afadhali kuwasubiri bandarini na kupanda mara melini kuwahudumia walionusurika katika safari, ingawa ilikuwa shida kutembea kati yao kwa jinsi walivyobanana.
 
Claver alivaa [[joho]] alilokuwa tayari kumpa yeyote mwenye shida; baadaye ilisemekana kwamba kila aliyelivaa alipona moja kwa moja maradhi yake.
 
Baada ya kushushwa ili kupangwa sokoni na kuuzwa baada ya umati wa wanunuzi kuwachunguzachunguza, Claver alikuwa anawapatia [[dawa]], [[chakula]], [[kileo]], [[limau]] na [[tumbaku]]. Kwa msaada wa [[wakalimani]] na [[picha]] kubwa aliyoleta, aliwapa mafundisho ya msingi katika [[imani]] ya [[Ukristo]].<ref name=ewtn>[http://www.ewtn.com/saintsHoly/saints/P/stpeterclaver.asp "St. Peter Claver"]</ref>
 
Claver alishindana na baadhi ya Wajesuiti wenzake waliokubali [[utumwa]], akahimiza wote kuwaona watumwa kama ndugu katika [[Kristo]]. Baada ya kuwafundisha na kuwabatiza alijitahidi wapate [[haki]] zao kama [[binadamu]] na kama [[Wakristo]].
 
Hata hivyo utume wake ulienea zaidi, kwa kuhubiri barabarani kwa ma[[baharia]] na [[wafanyabiashara]] pamoja na kwenda vijijini mpaka wakati wa kurudi kuwatembelea aliowabatiza na kuwatetea.
 
Wakati wa safari hizo, alikuwa anajitahidi kukwepa mapokezi ya wenye mashamba na wanyapara wao, akipendelea kulala katika makazi ya watumwa.
 
Vilevile alihudumia waliotembelea Cartagena (hata [Waprotestanti]] na [[Waislamu]]) na waliohukumiwa [[adhabu ya kifo]], ambao amewaandaa wengi kufa vizuri kiroho; pia alitembelea mara nyingi [[hospitali]] za mji huo.
 
Mwaka hadi mwaka, kazi na ushuhuda wake vilileta nafuu fulani katika hali ya watumwa, naye akawa na sauti iliyosikika.
 
[[File:038 Bones of San Pedro Claver in Cathedral.JPG|thumb|Mifupa ya Claver chini ya [[altare]] ya kanisa lake huko Cartagena]]
 
Miaka ya mwisho, Petro alikuwa [[mgonjwa]] mno asiweze kutoka chumbani. Kwa miaka 4 alibaki karibu peke yake, akihudumiwa vibaya (hata karibu kuachwa bila chakula) na mtumwa aliyekombolewa ambaye mkubwa wa nyumba alimuagiza kumshughulikia. Petro hakulalamika kamwe, akikubali yote kama [[malipizi]] ya [[dhambi]] zake.<ref name=ignatian>[http://www.ignatianspirituality.com/ignatian-voices/16th-and-17th-century-ignatian-voices/st-peter-claver-sj/ "St. Peter Claver, S.J.", Ignatian Spirituality]</ref> He died on 8 September 1654.
 
Watu wa Cartagena walipopata habari ya kifo chake, walilazimisha waruhusiwe kuingia chumbani ili kumpa [[heshima]] ya mwisho. Kutokana na sifa zake, walijipatia vipande vya nguo zake kama [[masalia]] hata karibu kumuacha uchi.<ref name=ignatian/>
 
Wakuu wa mji, ambao awali walimuona anawasumbua daima kwa kutetea watumwa, waliagiza [[mazishi]] ya fahari.
 
Alitangazwa mtakatifu pamoja na [[Alfonso Rodriguez]], na baada ya miaka minane [[1896]] Papa Leo XIII alimtangaza pia msimamizi wa umisionari wote katika ya Waafrika.<ref name=suau/>
 
Mwili wake unatunzwa katika [[kanisa]] la Wajesuiti alipokuwa anaishi, ambayo sasa linaitwa kwa jina lake.<ref>[http://www.lonelyplanet.com/colombia/caribbean-coast/cartagena/sights/museum/convento-san-pedro Lonely Planet "Cartagena Sights"]</ref>
 
==Tanbihi==