Ujamaa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 12:
# Kukuza kujitegemea kwa Tanzania kwa njia mbili: mabadiliko ya kiuchumi na mitazamo ya ki[[utamaduni]]. Kiuchumi, kila mtu angekifanyia kikundi chote kazi na kujifanyia yeye mwenyewe; kiutamaduni, ni lazima Watanzania wajifunze kujikomboa kutoka kwa [[utegemezi]] wa nchi za [[Ulaya]]. Kwake Nyerere, hii ilijumuisha Watanzania kujifunza kujifanyia mambo wao wenyewe na kujifunza kuridhika na kile ambacho wangeweza kufikia kama [[nchi huru]].
# Utekelezaji wa elimu bila malipo na ya lazima kwa Watanzania wote ili kuwahamasisha wananchi kuhusu kanuni za Ujamaa<ref name="Cranford"></ref>.
 
Uongozi wa Julius Nyerere uliivutia Tanzania macho na heshima ya kimataifa kutokana na msisitizo wake wa [[maadili]] kama msingi wa maamuzi ya [[siasa]]. Chini ya Nyerere Tanzania ilipiga hatua kubwa katika vipengele mbalimbali vya maendeleo: vifo vya watoto vilipungua kutoka 138 kwa 1000 waliozaliwa hai mwaka [[1965]] hadi 110 mwaka 1985; [[tarajio la kuishi]] lilipanda kutoka miaka 37 ([[1960]]) hadi 52 ([[1984]]); uandikishaji wa wanafunzi katika shule ya msingi ulipanda kutoka 25% (16% tu kwa watoto wa kike) mwaka 1960 hadi 72% (85% kwa watoto wa kike) mwaka 1985 (ingawa idadi ya wananchi ilikuwa inaongezeka kwa kasi); asilimia ya watu wazima waliojua kusoma na kuandika ilipanda kutoka 17% mwaka 1960 hadi 63% mwaka [[1975]] (juu sana kuliko nchi nyingine za Afrika) ikaendelea kupanda.<ref name="mwalimu">{{cite book | url= http://books.google.com.ar/books?id=ASWWRgOqk78C&pg=PA141&dq=mwalimu+the+influence+of+nyerere+preventive+detention+act&hl=es&ei=yh2HTa_CJ9TAtgfC083EBA&sa=X&oi=book_result&ct=result&resnum=1&ved=0CCgQ6AEwAA#v=onepage&q&f=false | title=Mwalimu: the influence of Nyerere | author=Colin Legum, G. R. V. Mmari}}</ref>
 
Hata hivyo Ujamaa (kama vile mipango mingine ya uzalishaji wa pamoja) ulipunguza uzalishaji hata kutia shaka juu ya uwezo wake wa kustawisha uchumi.<ref>[http://www.bbc.co.uk/news/magazine-20171366 Martin Plaut, "Africa's bright future"], ''BBC News Magazine'', 2 November 2012.</ref>
 
Hatimaye sababu mbalimbali zilifanya Ujamaa uonekane umeshindikana kiuchumi. Kati ya hizo, tatizo la kimataifa la [[mafuta]] [[miaka ya 1970]], anguko la bei ya bidhaa zilizozalishwa nchini (hasa [[kahawa]] na [[katani]]), utovu wa [[uwekezaji]] kutoka nje ya nchi na [[vita vya Uganda-Tanzania]] miaka [[1978]]-[[1979]] vilivyofyonza sana [[mtaji]] muhimu, na miaka miwili mfululizo ya [[ukame]].
 
Kufikia mwaka 1985 ilikuwa wazi kwamba Ujamaa ulishindwa kutoa Tanzania nje ya [[ufukara]] wake; Nyerere alitangaza kuwa atang'atuka asigombee tena [[urais]] katika uchaguzi wa mwaka huohuo.
 
==Hoja dhidi yake==
Line 64 ⟶ 72:
==Tanbihi==
<references></references>
 
==Marejeo==
* [[Paul Collier]]: ''Labour and Poverty in Rural Tanzania. Ujamaa and Rural Development in the [[United Republic of Tanzania]]''. New York: Oxford University Press, 1991, ISBN 0-19-828315-6{{Please check ISBN|reason=Check digit (6) does not correspond to calculated figure.}}.
 
==Viungo vya nje==