Tofauti kati ya marekesbisho "Fioretti"

403 bytes added ,  miaka 6 iliyopita
no edit summary
'''Fioretti''' (kwa [[Kiitalia]] maana yake ni '''Maua Madogo''', yaani '''Visimulizi Bora''') ni [[kitabu]] maarufu kuhusu [[Fransisko wa Asizi]] na wenzake kilichotafsiriwa mwishoni mwa [[karne ya 14]] kutoka kile cha [[Kilatini]] '''Actus beati Francisci et sociorum eius,''' kinachodhaniwa kuwa kiliandikwa na [[Ugolino Brunforte]] ([[1262]] hivi – [[1348]] hivi).
 
Ingawa hakizingatiwi sana kama chanzo cha kihistoria,<ref>[[Madeleine L'Engle]], and W. Heywood. ''The Little Flowers of St. Francis of Assisi''. New York: Vintage Spiritual Classic, 1998</ref> kimekuwa na sifa kuliko vitabu vingine juu ya [[mtakatifu]] huyo, kwa uzuri mkubwa upande wa [[lugha]] na [[usanii]] katika kusimulia. Ni kama [[manukato]] yanayotuvutia kwenye [[roho]] na [[utakatifu]] wa Fransisko, aliyekwishakufa toka siku nyingi, hivi kwamba anakumbukwa kwa mbali lakini kwa namna ya kupendeza zaidi. Miaka iliyopita imechuja [[ujumbe]] wake, ambao hivyo unang’aa kwa namna ya pekee katika kitabu hicho kilichosisitiza jinsi Fransisko alivyofanana na [[Yesu]], wazo lililokazwa na [[Wafransisko]] wote wa karne XIV.
 
==Filamu==