Volkeno : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
nyongeza kidogo
No edit summary
Mstari 11:
 
==Volkeno hai na volkeno bwete==
Volkeno inaweza kutokeakupatikana kama volkeno hai inayoendelea kutema moto, gesi na majivu. Inaweza pia kuonekana kama volkeno bwete inayokaa kama milima mingine bila kuonyesha dalili za moto. Lakini kutokana na umbo na tabia za miamba yake inaonekana mlima huu ulijengwa kwa njia ya kivolkeno.
 
Volkeno bwete inaweza kuamka tena. Mara nyingi kuwepo kwa chemchemi za maji ya moto au kutokea kwa gesi kwenye sehemu fulani ni dalili ya kwamba bado kuna njia kati ya mlima na magma ya chini. Kipindi kati ya milipuko kinaweza kuwa miaka mingi.