Beda Mheshimiwa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 1:
[[Image:Nuremberg Chronicle Venerable Bede.jpg|thumb|Beda Mheshimiwa alivyochorwa katika [[Kumbukumbu za Nuremberg]].]]
[[Picha:Bede.jpg|thumb|225px|right|[[Kaburi]] la Beda katika [[kanisa kuu]] la [[Durham]].]]
'''Beda''' maarufu kama '''Mheshimiwa''' tangu enzi za uhai wake (Wearmouth-Jarrow, leo nchini [[Uingereza]], [[672]] au [[673]] – [[25 Mei]] - Wearmouth-Jarrow, [[735]]) alikuwa [[mmonaki]], [[padri]], [[mwanateolojia]] na [[mwanahistoria]] [[nchi]]ni [[Uingereza]].
 
Hasa anafahamika kwa kitabu chake “Historia ya kikanisa ya taifa la Waingereza” (kwa [[Kilatini]]: ''Historia ecclesiastica gentis Anglorum''). Akiona [[Kanisa]] lilivyozidi kustawi kati ya mataifa mapya, alipenda kuonyesha lisivyobanwa na [[ustaarabu]] mmoja, bali linakumbatia kila aina ya [[utamaduni]] ili kuikamilisha katika [[Kristo]].
 
Mwaka [[1899]] alitangazwa na [[Papa Leo XIII]] kuwa [[mtakatifu]] na [[mwalimu wa Kanisa]].
Mstari 16:
Beda hasemi kitu kuhusu asili yake, lakini kuna dalili kuwa [[familia]] yake ilikuwa na hali nzuri katika jamii.
 
Kumbe anataja mahali alipozaliwa kama "maeneo ya monasteri hii", yaani monasteri pacha ya Wearmouth na Jarrow, [[Northumbria]], leo Uingereza Kaskazini Mashariki.
 
[[Abati]] wake wa kwanza alikuwa [[Benedikto Biscop]].
 
Alipofikia umri wa miaka 7, alitumwa monasterini ili apate [[malezi]] kutoka kwa abati huyo, halafu kwa [[Ceolfrith]]. Beda haelezi kama lengo la awali lilikuwa awe [[mmonaki]] baadaye. Lakini ndivyo ilivyotokea, akatumia maisha yake yote huko “kuimbia sifa za [[Mungu]], kusoma, kufundisha na kuandika”, alivyosema mwenyewe.
 
Alipofikia miaka 19 tu, ([[692]] hivi), alipewa [[daraja takatifu]] ya [[ushemasi]], na alipofikia miaka 30 ([[702]] hivi) alipata [[upadrisho]].
 
[[Mtaalamu]] wa [[biolojia]] na [[historia]], lakini hasa [[teoloja]], alifaulu kufanya [[Biblia]] ieleweke kwa urahisi kupitia mahubiri yake sahili iliyofuata mfano wa ma[[babu wa Kanisa]].
 
Alipata kuwa kati ya wasomi wakuu wa [[Karne za Kati]] za mwanzo, akifaidika na ma[[gombo]] mengi muhimu aliyoletewa na maabati wake kutoka [[safari]] zao nyingi za [[ng’ambo]].
 
[[Sifa]] ya [[ufundishaji]] na [[uandishi]] wake ilisababisha afanye [[urafiki]] na watu bora kadhaa wa wakati huo, ambao walimtia [[moyo]] kudumu kati kazi hiyo kwa faida ya wengi.
 
Mwaka [[701]] hivi aliandika vitabu vyake vya kwanza, ''De Arte Metrica'' na ''De Schematibus et Tropis''; vyote viwili kwa ajili ya madarasa.
 
Aliendelea kuandika maisha yake yote, akimaliza vitabu zaidi ya 60, vingi vikiwepo hadi leo.
 
[[Biblia]] ilikuwa daima chanzo kikuu cha [[teolojia]] yake. Baada ya kuchunguza [[nakala]] ipi ni sahihi zaidi, aliifafanua Kikristo, akijitahidi kuelewa vizuri maneno yanasema nini, lakini kwa [[mwanga]] wa Kristo aliye [[ufunguo]] wa Maandiko yote katika [[umoja]] wake wa dhati. Kwake matukio ya [[Agano la Kale]] na [[Agano Jipya]] yanakwenda pamoja kuelekeza kwa Kristo.
 
Mada nyingine aliyoipenda sana ni [[historia ya Kanisa]], kutokana na [[imani]] ya kwamba [[Roho Mtakatifu]] anazidi kufanya [[kazi]] ndani yake. Hivyo alipitia wakati wa [[Mitume wa Yesu|Mitume]], halafu [[Mababu wa Kanisa|Mababu]] na [[Mitaguso mikuu]] sita ya kwanza na kulinganisha [[tarehe]] za matukio mengi na [[ujio]] wa [[Yesu Kristo]], akichangia kufanya wote wakubali [[kalenda]] iliyoenea kila mahali, ikihesabu miaka kuanzia Kristo.
 
Vilevile alihesabu kitaalamu tarehe sahihi ya [[Pasaka]], iliyo [[kiini]] cha mwaka mzima wa [[liturujia]], akihimiza [[Wakristo]] wenyeji wa Uingereza na [[Ireland]] wakubali wote [[utaratibu]] wa [[Roma]] kuhusu mambo hayo. Kweli alichangia kuunganisha katika Ukristo mataifa yote ya [[Ulaya]].
 
[[Hotuba]] zake zilifaulu kuongoza waamini waadhimishe vema mafumbo ya imani na kuyatekeleza maishani, huku wakitarajia [[ujio wa pili]] wa [[Yesu]] ili kuingizwa naye katika [[liturujia ya mbinguni]].
 
Akifuata masisitizo ya Mababu kama [[Ambrosi]], [[Augustino]] na [[Sirili]], alifundisha kwamba [[sakramenti]] hazimfanyi mtu “awe Mkristo tu, bali Kristo mwenyewe”. Kila anayepokea kwa imani [[Neno la Mungu]] kwa mfano wa [[Bikira Maria]] anaweza kumzaa Kristo upya. Na Kanisa, kila linapobatiza watu, linakuwa “[[Mama wa Mungu]]” kwa kuwazaa kwa njia ya [[Roho Mtakatifu]].
 
Alihimiza [[walei]] wawe na [[bidii]] katika kupata mafundisho ya [[dini]] na kuwashirikisha mapema [[watoto]] wao. Pia wasali mfululizo kwa kutolea matendo yao yote kama [[sadaka ya kiroho]] pamoja na Kristo.
 
[[Mwanashairi]], aliandika tenzi kwa [[Bikira Maria]] ambazo ni kati ya zile bora zaidi zilizowahi kuandikwa.
Line 35 ⟶ 51:
 
Mwaka [[733]] alisafiri hadi [[York]], [[Lindisfarne]] na sehemu nyingine.
 
Alipougua, hakuacha kazi yake, akidumisha [[furaha]] ya dhati iliyojitokeza katika kusali na kuimba.
 
Alifariki tarehe 26 Mei 735 akazikwa Jarrow lakini masalia yake yakahamishiwa kwenye [[kanisa kuu]] la [[Durham]] katika [[karne ya 11]].
Line 100 ⟶ 118:
 
{{DEFAULTSORT:Bede Mheshimiwa}}
[[Jamii:WaliofarikiWaliozaliwa 735672]]
[[Jamii:Waliofariki 735]]
[[Jamii:Wabenedikto]]
[[Jamii:Mapadri]]
[[Jamii:Waliofariki 735]]
[[Jamii:Watakatifu wa Uingereza]]
[[Jamii:Walimu wa Kanisa]]