Umwagiliaji : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Addbot (majadiliano | michango)
d Bot: Migrating 70 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q11453 (translate me)
+ viungo
Mstari 6:
[[Picha:PivotIrrigationOnCotton.jpg|thumbnail|200px|Umwagiliaji wa [[pamba]] kwa njia ya [[kinyunyizo]] kikubwa kinachozunguka nchani]]
 
'''Umwagiliaji''' ni mtindo wa [[kilimo]] wa kupeleka [[maji]] kwa mimea shambani pasipo na [[mvua]] ya kutosha.
 
Hutumiwa katika maeneo [[yabisi]] au wakati mvua ni kidogo. Katika nchi baridi unatumiwa pia kwa kusudi la kulinda mazao dhidi ya [[jalidi]].
Mstari 13:
Umwagiliaji hutumia maji kutoka vyanzo mbalimbali:
* maji hutolewa kutoka [[mto]]ni au [[ziwa]]ni
* mwendo wa [[mto]] huzuiliwa kwa [[lambo]] na maji kutolewa katika ziwa ya lambo
* [[pampu]] yavuta maji kutoka [[kisima]]
 
== Mbinu za umwagiliaji ==
Mstari 27:
 
* Matumizi ya maji yanazidi akiba yake; mito imekauka kwa sababu watu wengi mno wamechukua maji mle. Mfano mbaya sana ni [[ziwa Aral]] iligeuzwa kuwa jangwa kwa sababu maji ya mito yake yametumiwa kwa miradi mikubwa ya pamba katika mazingira ya joto kali tena kwa teknolojia isiyofaa kama mifereji iliyo wazi
* Maji mengi yanapotea hasa pale ambako maji hupitishwa kwenye mifereji au na kujaza shamba kumwagiliwa kwa [[vinyunyizo]]. Sehemu kubwa inapotea kwa njia ya [[uvukizaji]] kuliko kulisha zao.
* Pampu zimesababisha kushuka kwa uwiano wa maji chini ya ardhi. Hi ni hofu kubwa kwa umwagiliaji katika jangwa [[Sahara]] unaotumia akiba ya maji iliyojengwa na mvua wa milenia nyingi lakini inayopungua haraka tangu kuanzishwa kwa miradi ya umwagiliaji kwa pampu kubwa zinazovuta maji ya chini.
* uharibifu wa mashamba ka kuongeza kiwango cha [[chumvi]] ardhini; katika mazingira ya joto uvukizaji wa maji unapeleka chumvi iliyoko ardhini juu; maji yavukiza lakini chumvi inabaki. Kuna mifano mingi ambako mashamba yameshaharibika kutokana na kuongezeka kwa chumvi. Maeneo yalisolishayaliyolisha watu tangu kale yamekuwa jangwa kabisa.
 
Matatizo haya yote yanaonyesha ya kwamba haitoshi kumwagilia mashamba tu na kufurahia mazao mazuri kwa sababu matatizo yataongezeka baada ya miaka kadhaa. Kwa hiyo ni lazima kuangalia vema mbinu za uimwagiliaji inayolingana na mazingira na kutumia maji kidogo kama vile umwagiliaji kwa matone.