Kihindustani : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 1:
'''Kihindustani''' (pia: '''Kihindi-Kiurdu''') ni lugha ya pamoja katika kaskazini ya [[Uhindi]] na [[Pakistan]]. Inapatikana kwa umbo sanifu tofauti katika kila nchi na hii ni [[Kiurdu]] katika Pakistan na [[Kihindi]] katika India.
 
Kinahesabiwa kuwa kati ya [[lugha za Kihindi-Kiajemi]] ndani ya [[lugha za Kihindi-Kiulaya.]]. Lugha za karibu ni pamoja [[Kipunjabi]], [[Kisindhi]], [[Kigujarati]], [[Kimarathi]] na [[Kibengali]].
 
Maandishi ni tofauti kila nchi yaani upande wa Pakistan kwa [[herufi za Kiarabu]] na upande wa Uhindi kwa herufi za [[Devanagari]]. Lakini kama lugha ya majadiliano hakuna tofauti. Sarufi ni sawa, lakini kuna kiasi cha tofauti katika msamiati hasa katika lugha ya maandishi. Upande wa Kiurdu / Pakistan kuna maneno mengi zaidi yenye asili ya [[Kiarabu]], [[Kituruki]] na [[Kiajemi]]. Upande wa Uhindi waandishi hutumia zaidi maneno yenye asili katika [[Kisanskrit]].