Yosia : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'thumb|right|Mfalme Yosia katika ibada hekaluni '''Yosia''', kwa Kiebrania יֹאשִׁיָּהוּ, Yoshiyyáhu|Yôšiyyāhû, maana ya...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 15:17, 18 Juni 2014

Yosia, kwa Kiebrania יֹאשִׁיָּהוּ, Yoshiyyáhu|Yôšiyyāhû, maana yake "aliyeponywa na YHWH" au "aliyetegemezwa na Yah"[1][2]; kwa Kigiriki Ιωσιας; kwa Kilatini Josias}}; (649 KK609 KK) alikuwa mfalme wa Yuda (641 KK – 609 KK) aliyejitahidi kufanya urekebisho upande wa dini ya Israeli ili kufuata zaidi Torati iliyoelekea kukamilika.

Mfalme Yosia katika ibada hekaluni

Mwana wa mfalme Amon na Jedidah[3], Yosia alirithi utawala akiwa mtoto wa miaka 8 tu, kutokana na uuaji wa baba yake, akatawala miaka 31,[4] kuanzia 641/640 KK to 610 KK/609 KK.[5]

Anatajwa katika Injili ya Mathayo kama babu wa Yesu.

Familia

Yosia anajulikana tu katika Biblia. Nje yake hatajwi popote.[6]

Babu yake, Manase anatajwa na Biblia kama mmojawapo kati ya wafalme waovu zaidi wa ukoo wa Daudi kwa jinsi alivyoelekeza raia zake kuacha ibada ya Mungu mmoja ili kufuata dini za mataifa makuu ya wakati huo, hata kutumia Hekalu la Yerusalemu, kinyume cha uaminifu wa baba yake Hezekia.

Yosia alizaa watoto wa kiume wanne: Yohane, Eliakimu[7], Matania na Shallum.[8]

Kwanza Shallum alimrithi Yosia kwa jina la Yehoahazi.[9] lakini baada ya miezi tu nafasi yake ilishikwa na Eliakimu kwa jina la Yehoyakimu,[10] halafu na mtoto wa huyo, Yekonia;[11] hatimaye alitawala Mattania kwa jina la Zedekia.[12] Huyo akawa malme wa mwisho wa Yuda kwa kushindwa na Babuloni akapelekwa uhamishoni huko pamoja na Wayahudi wengi mwaka 586 KK.

Tanbihi

  1. Josiah definition - Bible Dictionary - Dictionary.com. Retrieved 25 July 2011.
  2. Wells, John C. (1990). Longman pronunciation dictionary. Harlow, England: Longman. uk. 386. ISBN 0-582-05383-8.  entry "Josiah"
  3. "Josiah", Jewish Encyclopedia
  4. 2Fal 22:1; 2Fal 21:23-26; 2Fal 21:26
  5. Edwin Thiele, The Mysterious Numbers of the Hebrew Kings, (1st ed.; New York: Macmillan, 1951; 2d ed.; Grand Rapids: Eerdmans, 1965; 3rd ed.; Grand Rapids: Zondervan/Kregel, 1983). ISBN 0-8254-3825-X, 9780825438257, 217.
  6. Alpert, Bernard; Alpert, Fran (2012). Archaeology and the Biblical Record. Hamilton Books. uk. 74. ISBN 978-0761858355. 
  7. 2 Kings 23:34
  8. 1Nya 3:15; 2Fal 23:36; 2Fal 24:18; 2Fal 23:31
  9. 1Nya 3:15; Yer 22:11
  10. 2Nya 36:4;
  11. 2Nya 36:8
  12. 2Fal 24:17

Marejeo

Viungo vya nje

Kigezo:Mtu-Biblia