Beda Mheshimiwa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 37:
Aliendelea kuandika maisha yake yote, akimaliza vitabu zaidi ya 60, vingi vikiwepo hadi leo.
 
[[Biblia]] ilikuwa daima chanzo kikuu cha [[teolojia]] yake. Baada ya kuchunguza [[nakala]] ipi ni sahihi zaidi, aliifafanua Kikristo, akijitahidi kuelewa vizuri maneno yanasema nini, lakini kwa [[mwanga]] wa Kristo aliye [[ufunguo]] wa Maandiko yote katika [[umoja]] wake wa dhati. Kwake matukio ya [[Agano la Kale]] na ya [[Agano Jipya]] yanakwenda pamoja kuelekeza kwa Kristo.
 
Mada nyingine aliyoipenda sana ni [[historia ya Kanisa]], kutokana na [[imani]] ya kwamba [[Roho Mtakatifu]] anazidi kufanya [[kazi]] ndani yake. Hivyo alipitia wakati wa [[Mitume wa Yesu|Mitume]], halafu [[Mababumababu wa Kanisa|Mababu]] na [[Mitaguso mikuu]] sita ya kwanza na kulinganisha [[tarehe]] za matukio mengi na [[ujio]] wa [[Yesu Kristo]], akichangia kufanya wote wakubali [[kalenda]] iliyoenea sasa kila mahali, ikihesabu miaka kuanzia Kristo.
 
Vilevile alihesabu kitaalamu tarehe sahihi ya [[Pasaka]], iliyo [[kiini]] cha mwaka mzima wa [[liturujia]], akihimiza [[Wakristo]] wenyeji wa Uingereza na [[Ireland]] wakubali wote [[utaratibu]] wa [[Roma]] kuhusu mambo hayo. Kweli alichangia kuunganisha katika Ukristo mataifa yote ya [[Ulaya]].
 
[[Hotuba]] zake zilifaulu kuongoza waamini waadhimishe vema mafumbo ya imani na kuyatekeleza maishani, huku wakitarajia [[ujio wa pili]] wa [[Yesu]] ili kuingizwa naye katika [[liturujia ya mbinguni]].
 
Akifuata masisitizo ya Mababumababu kama [[Ambrosi]], [[Augustino]] na [[Sirili]], alifundisha kwamba [[sakramenti]] hazimfanyi mtu “awe Mkristo tu, bali Kristo mwenyewe”. Kila anayepokea kwa imani [[Neno la Mungu]] kwa mfano wa [[Bikira Maria]] anaweza kumzaa Kristo upya. Na Kanisa, kila linapobatiza watu, linakuwa “[[Mama wa Mungu]]” kwa kuwazaa kwa njia ya [[Roho Mtakatifu]].
 
Alihimiza [[walei]] wawe na [[bidii]] katika kupata mafundisho ya [[dini]] na kuwashirikisha mapema [[watoto]] wao. Pia wasali mfululizo kwa kutolea matendo yao yote kama [[sadaka ya kiroho]] pamoja na Kristo.