Karatasi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Addbot (majadiliano | michango)
d Bot: Migrating 118 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q11472 (translate me)
Mstari 40:
Watu wa [[Meksiko ya Kale]] walitengeneza laha za amatl. Hapa walitumia ganda laini ya ndani ya miti aina za [[mibuyu]] lililochemshwa na kupigwa hadi kuwa laha.
 
===Karatasi kutoka China==
Karatasi yenyewe ilibuniwa nchini China. Waziri Tsai-Lun alieleza mnamo mwaka [[105]] mtindo wa kutengeneza karatasi katika kitabu chake. Mabaki ya [[hariri]] yalichanganywa na nguo zilizochakaa na [[utembo]] wa miti. Yote yalipondwa na kusagwa halafu kupikwa katika maji na kusafishwa. Nyuzi tupu zilizobaki zilichotwa kwa chujio halafu zikaslibiwa ndani ya chujio na kukandamizwa na kukaushwa.