Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d Masahihisho aliyefanya 5.153.28.70 (Majadiliano) yalirejeshwa hadi sahihisho la mwisho na Riccardo Riccioni
wikinger RAHOWA 1488
Mstari 1:
R A H O W A
[[Picha:Map 1914 WWI Alliances.jpg|thumb|Shirikiano za kijeshi katika Ulaya mwaka 1915. Nyekundu: [[Mataifa ya Kati]]; kijani: [[Mataifa ya Ushirikiano]]; njano: mataifa yasiyoshiriki vita|271x271px]]
[[Picha:WWImontage.jpg|thumb|350 px|right|Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia: <br />1.Mifereji huko Verdun (Ufaransa) baada ya kulimwa kwa mizinga mikubwa; <br />2. Ndege za kijeshi na faru za kwanza; <br />3. bunduki ya mtombo na manowari ]]
[[Picha:WWI.png|thumb|400px|Ramani ya dunia ikionyesha nchi na maeneo yaliyoshiriki katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Kijani: [[Mataifa ya Ushirikiano]]; njano: [[Mataifa ya Kati]]; nchi zisizoshiriki kwa rangi ya kijivu]]
 
'''Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia''' ilikuwa vita iliyopigwa kuanzia mwaka [[1914]] hadi [[1918]]. Mataifa wapiganaji yalikuwa [[Ujerumani]], [[Austria-Hungaria]], [[Bulgaria]] na [[Uturuki]] (ziliitwa "Mataifa ya Kati") kwa upande mmoja dhidi ya [[Ufaransa]], [[Urusi]], [[Uingereza]], [[Italia]], [[Marekani]] na nchi mbalimbali zilizoshirikiana nazo (zilitwa "Mataifa ya Ushirikiano").
 
Vita hii ilianza katika [[Ulaya]] ikapanuka haraka hadi [[Mashariki ya Kati]], [[Afrika]] na [[Asia ya Mashariki]] ikasababisha [[kifo]] cha takriban watu milioni tisa.
 
== Sababu na matokeo ==
'''Sababu yake''' ilikuwa mashindano makali kati ya mataifa ya [[Ulaya]] kuhusu kushika nafasi ya [[kipaumbele]] barani Ulaya na duniani kote.
 
'''Matokeo yake''' yalikuwa mwisho wa kipaumbele cha Ulaya duniani na kupanda ngazi kwa Marekani, [[mapinduzi]] katika nchi mbalimbali, mwisho wa falme za Ujerumani, [[Austria]] na Urusi pamoja na mwanzo wa utawala wa [[Ukomunisti|kikomunisti]] katika Urusi, mwisho wa Dola la Austria-Hungaria na wa [[Dola la Uturuki]] la Kiosmani pamoja na mwisho wa [[ukoloni]] wa Kijerumani duniani.
 
Katika Ulaya '''nchi mpya''' zilijitokeza kama vile [[Chekoslovakia]], [[Finland]], [[Latvia]], [[Estonia]] na [[Yugoslavia]] pamoja na nchi za zamani zilizotokea tena katika uwanja wa kimataifa ndizo [[Austria]], [[Hungaria]], [[Lithuania]] na [[Poland]].
 
== Hali kabla ya vita ==
Sehemu kubwa ya Ulaya iliwahi kuwa na kipindi kirefu cha [[amani]] tangu vita kati ya Ufaransa na Ujerumani mnamo [[1870]]-[[1871]]. Mataifa ya Ulaya yalikuwa na mfumo wa mikataba na mapatano kati yao yaliyolenga kuhakikisha uwiano wa mataifa. Mataifa makubwa ya Ulaya yalikuwa Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Urusi na Italia.
 
Hali ilikuwa tofauti katika Kusini-Mashariki mwa bara hilo. Hadi nusu ya pili ya [[karne ya 19]] sehemu kubwa ya [[Balkani]] ilitawaliwa na [[Milki ya Osmani]] iliyokuwa milki ya [[Uislamu|Kiislamu]] ya kutawala [[Wakristo]] wengi. Milki hiyo iliendelea kudhoofika na kuacha nchi ndogo kujipatia [[uhuru]], kama vile [[Ugiriki]].
 
== Mwanzo wa vita ==
Vita ilianza kutokana na [[ugomvi]] kati ya Austria-Hungaria na [[Serbia]]. Kutokana na muundo wa mikataba ya kusaidiana kati ya nchi za Ulaya mwanzo huo ulisababisha mfululizo wa hali ya vita kati ya mataifa, na mengine ya Balkani yalitafuta uhuru wao.
 
Tarehe [[28 Juni]] [[1914]] katika [[mji]] wa [[Sarayevo]], [[Bosnia]], [[mwana]] wa [[Kaisari]] wa Austria aliyekuwa mfalme mteule aliuawa pamoja na [[mke]] wake na [[gaidi]] [[Mserbia]] mwanachama wa kundi la "[[Mkono Mweusi]]" lililopinga utawala wa Austria-Hungaria katika [[Bosnia]]. Austria ilidai [[Serbia]] ifuate masharti makali katika [[uchunguzi]] wa tendo lile. Serbia ilipokataa sehemu ya masharti, Austria ilitangaza hali ya vita dhidi ya Serbia tarehe [[28 Julai]] [[1914]].
 
Agosti ya 1914 iliona kupanuka kwa vita hii: Warusi walikuwa na mkataba wa usaidizi na Serbia wakatangaza hali ya vita dhidi ya Austria-Hungaria. Hapo wakaingia Wajerumani waliokuwa na mapatano ya usaidizi na Austria-Hungaria wakitangaza hali ya vita dhidi ya Urusi. Urusi kwa upande wake ulikuwa na mkataba wa kusaidiana na Ufaransa, hivyo hali ya vita ikajitokeza pia kati ya Ufaransa na Ujerumani. Uingereza ulijiunga na vita baada ya Wajerumani kuanza kuingia eneo la [[Ubelgiji]] kwa shabaha ya kuvuka haraka ili wavamie Ufaransa Kaskazini.
 
Kuanzia Oktoba 1914 [[Milki ya Osmani]] ([[Uturuki]]) ilijiunga na vita kufuatana na mkataba wake wa siri na Ujerumani.
 
Mwaka [[1915]] Italia ilijiunga na Wafaransa na Waingereza kwa kushambulia Austria-Hungaria, ingawa awali ilikuwa na mkataba na [[dola]] hilo.
 
== Vita katika nchi mbalimbali ==
 
Vita ilipigwa kwa ukali miaka ya 1914-1918. Wajerumani waliingia ndani ya Ufaransa lakini walikwama kabla ya kufikia [[mji mkuu]] wa [[Paris]]. Kwa muda mrefu mstari wa mapambano ulibaki palepale.
 
Katika Mashariki Wajerumani walifaulu kurudisha mashambulio ya Kirusi na kuteka sehemu za Urusi.
Katika Kusini mwa Ulaya Waustria walifaulu kwa shida kubwa kuteka Serbia na [[Montenegro]] pamoja na [[Albania]].
 
Waturuki walishindwa kwa ujumla katika mashambulio yao dhidi ya Warusi katika eneo la [[Kaukazi]] na dhidi ya Waingereza katika [[Misri]]. Lakini walifaulu kuzuia Waingereza wasifike Uturuki penyewe. Waingereza walipeleka jeshi katika [[Irak]] ya kusini wakafaulu kuwarudisha Waturuki hadi kaskazini ya nchi hii.
 
== Vita katika makoloni ==
Vita ilienea haraka [[bahari]]ni na katika makoloni ya Ujerumani yaliyovamiwa na Waingereza, Wafaransa, [[Afrika Kusini]] na [[Japani]]. Makoloni yalikuwepo [[Afrika]] na kwenye [[visiwa vya Pasifiki]] pamoja na [[China]]. Ujerumani ilikuwa na vikosi vya kijeshi katika makoloni ya Afrika na pia huko [[Qingdao]] nchini [[China]].
 
Kwa ujumla makoloni yote yasiyokuwa na [[jeshi]] yalitekwa na mataifa ya ushirikiano bila mapigano.
* [[Afrika ya Kusini-Magharibi ya Kijerumani]] ilivamiwa na Afrika Kusini na [[jeshi la ulinzi la Kijerumani]] likajisalimisha mnamo Julai 1915.
* [[Kamerun]] ilivamiwa na Ufaransa na Uingereza kutoka makoloni yao ya [[Nigeria]] na [[Afrika ya Kati ya Kifaransa]]. Jeshi la ulinzi likajisalimisha katika Februari [[1916]].
* [[Afrika ya Mashariki ya Kijerumani]] ilikuwa mahali pa mapigano yaliyoendelea kwa miaka yote ya vita. Jeshi la Ulinzi wa Kijerumani chini ya uongozi wa [[Paul von Lettow-Vorbeck]] lilifaulu kutetea eneo la koloni dhidi ya mashambulio ya kwanza ya Waingereza kutoka [[Kenya]] hadi 1916. Kwenye Novemba 1914 jeshi la [[askari]] 8,000 kutoka [[Uhindi]] lilishindwa kwenye [[mapigano ya Tanga]]. Hadi mwanzo wa 1916 Waingereza walikusanya jeshi kubwa kutoka Afrika Kusini na Uhindi wakafaulu kutwaa sehemu kubwa ya koloni hadi Agosti 1916. Jeshi la ulinzi likaendelea kushika sehemu ya kusini ya koloni hadi [[1917]] ilipopaswa kuhamia eneo la [[Ureno|Kireno]] katika [[Msumbiji]]. Waingereza na Wareno walishindwa kulishika kundi la Kijerumani. Mwaka 1918 Lettow-Vorbeck alirudi [[Tanganyika]] akaingia [[Rhodesia ya Kaskazini]] alipoambiwa na Waingereza mnamo Novemba 1918 ya kwamba vita ya Ulaya ilikwisha tayari.
 
== Mwisho wa vita ==
Wakati 1917 mataifa ya Ulaya yalionyesha [[dalili]] za [[uchovu]]. Katika hali hiyo ma[[badiliko]] mawili makubwa yalitokea: Marekani ilijiunga na vita dhidi ya Wajerumani na Urusi uliona mapinduzi yaliyolazimisha [[serikali]] mpya kutia [[sahihi]] mapatano ya kumaliza mapigano dhidi ya Wajerumani walioteka maeneo makubwa ya Urusi.
 
Nguvu ya Marekani ilionekana haraka na [[bahati]] ya Ujerumani ilipungua sana. Austria-Hungaria ilidhoofishwa vilevile.
 
Mwaka 1918 iliona mwisho wa vita. Milki za Austria na Uturuki zilikwisha zikagawiwa na sehemu zao zilikuwa nchi mpya au nchi zilizoundwa upya.
 
== Mkutano wa Paris ==
Mwaka [[1919]] mataifa washindi walikutana Paris (Ufaransa) wakikubaliana ma[[sharti]] ya kumaliza hali ya vita dhidi ya Mataifa ya Kati. Mikataba mbalimbali iliandaliwa kati ya washindi na kuwekwa mbele ya nchi zilizoshindwa.
 
Mikataba hii ilikuwa:
* [[Mkataba wa Versailles]] na Ujerumani ([[28 Juni]] [[1919]]),
* [[Mkataba wa Saint-Germain]] na Austria ([[10 Septemba]] 1919),
* [[Mkataba wa Neuilly]] na Bulgaria ([[27 Novemba]] 1919),
* [[Mkataba wa Trianon]] na Hungaria ([[4 Juni 1920]]),
* [[Mkataba wa Sèvres]] na [[Milki ya Osmani]] ([[Uturuki]]) ([[10 Agosti]] 1920; ukasahihishwa na [[mkataba wa Lausanne]] ([[24 Julai]] [[1923]]).
Mkutano wa Paris ulitoa masharti makali dhidi ya Ujerumani katika [[Mkataba wa Versailles]]. Ujerumani uliondolowa makoloni yote yaliyokabidhiwa kwa niaba ya [[Shirikisho la Mataifa]] kama [[maeneo ya kukabidhiwa]] kwa Uingereza, Ufaransa, Ubelgiji, Japani, [[Afrika Kusini]] na [[Australia]].
 
Mkutano wa Paris ulikuwa jaribio la kuunda [[utaratibu]] mpya duniani uliotakiwa kulindwa na Shirikisho la Mataifa. Lakini ukosefu wa nguvu kwa upande wa Shirikisho la Mataifa pamoja na kuanza na kupanuka kwa mwendo mpya wa [[Ufashisti|Kifashisti]] iliyochukua utawala katika Italia na Ujerumani vilishinda nia hiyo.
 
[[Wataalamu]] wasio wachache wanasema mwisho wa vita kuu ya kwanza ulipanda tayari [[mbegu]] za [[Vita Kuu ya Pili ya Dunia]].
 
Ni kwamba Wajerumani na wakazi wa nchi nyingine zilizoshindwa walijiona wamekosewa haki, lakini pia Waitalia walioshinda kwa gharama kubwa ya [[damu]] walijiona wamedanganywa kwa kutotimiziwa [[ahadi]] walizopewa ili wasaliti Ujerumani na Austria-Hungaria na kuingia vitani upande wa pili. Hivyo vyama vya [[mrengo wa kulia]] viliweza kupata nguvu na hatimaye kupanga [[kisasi]].
 
==Vita ya kwanza ya dunia?==
Vita hii ilitwa "Vita ya Dunia" kwa sababu mapigano yalisambaa kote duniani. Sehemu kubwa ya mapigano yalitokea Ulaya na Asia ya Magharibi lakini pia katika makoloni ya Afrika, Asia na Pasifiki. Nchi za Amerika hazikuona mapigano kwenye [[nchi kavu]] lakini [[manowari]] za Ujerumani zilipigana na mataifa ya ushirikiano mbele ya [[pwani]] za Marekani na [[Amerika Kusini]].
 
Ilikuwa pia vita ya kwanza iliyopigwa kote duniani ilhali habari zake ziliweza kufika katika muda wa masaa au siku chache kwa mataifa yote kutokana na upatikanaji wa vyombo vya mawasiliano hasa [[simu]] za kimataifa na [[redio]].
 
Lakini kwa kweli haikuwa vita ya kwanza ya "dunia" maana [[vita ya miaka saba]] ([[1756]]-[[1762]]) ilipigwa pia kwenye mabara yote ya dunia baina ya nchi zenye makoloni hasa Uingereza, Ufaransa na [[Hispania]].
 
== Viungo vya nje ==
* [http://www.firstworldwar.com/ Historia ya Vita Kuu ya Kwanza (Kiingereza)]
 
[[Jamii:Vita]]
[[Jamii:Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia|*]]
[[Jamii:Historia ya Ulaya]]
[[Jamii:Historia]]
 
{{Link FA|ast}}
{{Link FA|de}}
{{Link FA|eo}}
{{Link FA|he}}
{{Link FA|ka}}
{{Link FA|ro}}
{{Link FA|sr}}
{{Link FA|vi}}