Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d Masahihisho aliyefanya 67.55.100.196 (Majadiliano) yalirejeshwa hadi sahihisho la mwisho na Nastoshka
nyongeza kidogo
Mstari 17:
Sehemu kubwa ya Ulaya iliwahi kuwa na kipindi kirefu cha [[amani]] tangu vita kati ya Ufaransa na Ujerumani mnamo [[1870]]-[[1871]]. Mataifa ya Ulaya yalikuwa na mfumo wa mikataba na mapatano kati yao yaliyolenga kuhakikisha uwiano wa mataifa. Mataifa makubwa ya Ulaya yalikuwa Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Urusi na Italia.
 
Hali ilikuwa tofauti katika Kusini-Mashariki mwa bara hilo. Hadi nusu ya pili ya [[karne ya 19]] sehemu kubwa ya [[Balkani]] ilitawaliwa na [[Milki ya Osmani]] iliyokuwa milki ya [[Uislamu|Kiislamu]] ya kutawala [[Wakristo]] wengi. Milki hiyohii iliendelea kudhoofika nawakati kuachawa nchikarne ndogoya kujipatia19. Nchi mbalimbali zilijitenga na kupata [[uhuru]], kama vile [[Ugiriki]], [[Serbia]], [[Bulgaria]] na [[Romania]]. Nchi hizi mpya zilipigana kivita kati yao na Milki ya Osmani hadi mwaka 1912.
 
== Mwanzo wa vita ==
Vita Kuu ilianza kutokana na [[ugomvi]] kati ya Austria-Hungaria na [[Serbia]]. Kutokana na muundo wa mikataba ya kusaidiana kati ya nchi za Ulaya mwanzo huo ulisababisha mfululizo wa hali ya vita kati ya mataifa, na mengine ya Balkani yalitafuta uhuru wao.
 
Tarehe [[28 Juni]] [[1914]] katika [[mji]] wa [[Sarayevo]], [[Bosnia]], [[mwana]] wa [[Kaisari]] wa Austria aliyekuwa mfalme mteule aliuawa pamoja na [[mke]] wake na [[gaidi|mgaidi]] [[Mserbia]] mwanachama wa kundi la "[[Mkono Mweusi]]" lililopinga utawala wa Austria-Hungaria katika [[Bosnia]]. Austria ilidai [[Serbia]] ifuate masharti makali katika [[uchunguzi]] wa tendo lile. Serbia ilipokataa sehemu ya masharti, Austria ilitangaza hali ya vita dhidi ya Serbia tarehe [[28 Julai]] [[1914]].
 
Agosti ya 1914 iliona kupanuka kwa vita hii: Warusi walikuwa na mkataba wa usaidizi na Serbia wakatangaza hali ya vita dhidi ya Austria-Hungaria. Hapo wakaingia Wajerumani waliokuwa na mapatano ya usaidizi na Austria-Hungaria wakitangaza hali ya vita dhidi ya Urusi. Urusi kwa upande wake ulikuwa na mkataba wa kusaidiana na Ufaransa, hivyo hali ya vita ikajitokeza pia kati ya Ufaransa na Ujerumani. Uingereza ulijiunga na vita baada ya Wajerumani kuanza kuingia eneo la [[Ubelgiji]] kwa shabaha ya kuvuka haraka ili wavamie Ufaransa Kaskazini.