Tofauti kati ya marekesbisho "Ruthu"

1,757 bytes added ,  miaka 6 iliyopita
no edit summary
d (Robot: Fixing double redirect)
[[File:A.Cortina Ruth.jpg|thumb|220px|''Ruthu'' alivyochorwa na [[Antonio Cortina Farinós]].]]
#REDIRECT [[Kitabu cha Ruthu]]
'''Ruthu''' ni mmojawapo kati ya [[wanawake]] wachache ambao ni wahusika wakuu wa [[kitabu]] kimojawapo cha [[Biblia]], kiasi cha kukipa [[jina]].
 
Katika fujo ya miaka ya [[Waamuzi]] (inayosimuliwa na [[Kitabu cha Waamuzi]]), habari ya kitabu hiki kifupi inatujenga: inahusu Ruthu, mwanamke [[Mpagani]] wa [[kabila]] la [[Moabu]] aliyeolewa na Mwisraeli kwao, huko ng’ambo ya [[mto]] [[Yordani]].
 
Baada ya kufiwa [[mume]] wake akafuatana na [[mama mkwe]] [[Naomi]] hadi [[Bethlehemu]] ili aolewe na [[ndugu]] wa [[marehemu]] na kumzalia [[mtoto]] kadiri ya [[Torati]], [[sheria]] ya [[Israeli]].
 
Baada ya kufanikiwa kuolewa na Boazi kwa msaada wa Naomi, alimzaa [[Obedi]].
 
Huyo mtoto akawa baba wa [[Yese]] na [[babu]] wa [[mfalme Daudi]].
 
Hivyo kwa uaminifu wake mwanamke huyo pia akatajwa katika [[Injili]] kama bibi wa [[Yesu]] ([[Math]] 1:5-6).
 
== Mazingira ==
 
Habari kuu ya kitabu cha Ruthu ilitokea wakati wa Waamuzi, lakini inafurahisha [[moyo]], ikilinganishwa na hali mbaya ya ki[[dini]] na ya ki[[maadili]] iliyoandikwa katika kitabu cha Waamuzi.
 
Habari yenyewe inaonyesha kwamba [[imani]] kamili kwa [[Mungu]] na uangalifu na [[upendo]] kwa watu wengine wakati ule pia ulikuwepo katika Israeli.
 
Katika [[taifa]] zima walikuwepo watu waliojitahidi kuishi maisha ya [[unyenyekevu]] na [[haki]] mbele ya Mungu wa kweli.
 
Habari hiyo pia inaonyesha kwamba Mungu aliwaangalia watu kama hao kwa [[neema]] yake kubwa, akiyaongoza mambo yao ya kila siku na kuwafanikisha. [[Wema]] huo pia ulikuwa [[baraka]] kwa taifa zima.
 
== Viungo vya nje ==
* [http://www.biblephone.net/mobile/index.php/swa/2/Ru/ Kitabu cha Ruth katika Biblia (Union Version)]
 
[[Jamii:Watu wa Biblia]]