Kanuni ya Imani : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'thumb|[[Picha takatifu ikimuonyesha Konstantino Mkuu (katikati) na wajumbe wa Mtaguso wa kwanza wa Nisea (325) wakishika Kan...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 14:26, 21 Septemba 2014

Kanuni ya imani, au Ungamo la imani, au Tamko la imani, au Nasadiki (Ukristo) au Shahada (Uislamu) ni fomula iliyopangwa kwa muhtasari ili wafuasi wa dini fulani wakiri kwamba wanaamini mafundisho ya dini hiyo.

Picha takatifu ikimuonyesha Konstantino Mkuu (katikati) na wajumbe wa Mtaguso wa kwanza wa Nisea (325) wakishika Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli ya mwaka 381.

Katika Uyahudi

Inajadiliwa kama dini ya Uyahudi ina kanuni ya imani. Baadhi wanasema ipo, nayo ni [[Shema Yisrael] (Kumb 6:4), inayoanza hivi: "Sikiliza, ee Israeli: Bwana Mungu wetu, Bwana ni mmoja."

Katika Ukristo

Katika Ukristo ni maarufu hasa Kanuni ya Imani ya Nisea Konstantinopoli, iliyotungwa mwaka 325 katika Mtaguso wa kwanza wa Nisea na kukamilishwa mwaka 381 katika Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli. Ndiyo ya kwanza katika ya Mitaguso ya kiekumene. Msingi wa fomula hiyo ni Agano Jipya lilivyoeleweka kwa kawaida na maaskofu wa Kanisa wa karne ya 4, ambayo ni muhimu sana katika ufafanuzi wa imani uliofanywa na mababu wa Kanisa. Karibu madhehebu yote ya Ukristo yanakubali hadi leo kanuni hiyo.[1]

Pamoja nayo inakubalika sana Kanuni ya Imani ya Mitume iliyotokea Roma katika maadhimisho ya liturujia, hasa ubatizo.

Katika Uislamu

Waislamu wanatamka maneno ya shahada kama nguzo mojawapo ya dini yao ili kumkiri Mungu pekee (Allah) na mtume Muhammad kama rasuli wake.[2]

Tanbihi

Marejeo

  • Christian Confessions: a Historical Introduction, [by] Ted A. Campbell. First ed. xxi, 336 p. Louisville, Ky.: Westminster/John Knox Press, 1996. ISBN 0-664-25650-3
  • Creeds and Confessions of Faith in the Christian Tradition. Edited by Jaroslav Pelikan and Valerie Hotchkiss. Yale University Press 2003.
  • Creeds in the Making: a Short Introduction to the History of Christian Doctrine, [by] Alan Richardson. Reissued. London: S.C.M. Press, 1979, cop. 1935. 128 p. ISBN 334-00264-8
  • Ecumenical Creeds and Reformed Confessions. Grand Rapids, Mich.: C.R.C. [i.e. Christian Reformed Church] Publications, 1987. 148 p. ISBN 0-930265-34-3
  • The Three Forms of Unity (Heidelberg Catechism, Belgic Confession, [and the] Canons of Dordrecht), and the Ecumenical Creeds (the Apostles' Creed, the Athanasian Creed, [and the] Creed of Chalcedon). Reprinted [ed.]. Mission Committee of the Protestant Reformed Churches in America, 1991. 58 p. Without ISBN

Viungo vya nje

  Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.