Atomu : Tofauti kati ya masahihisho

476 bytes added ,  miaka 8 iliyopita
no edit summary
(sahihisho)
No edit summary
[[Picha:Atom.png|thumb|Mfumo wa atomi kwa mfano wa atomi ya [[Heli]]: [[Elektroni]] mbili (njano) kwenye mzingo wa atomi huzunguka kiini chenye [[Protoni]] mbili (nyekundu) na [[Neutroni]] mbili (kijani).]]
 
'''Atomi''' (pia: '''atomu'''; kutoka [[kigiriki]] '''ἄτομος''' ''átomos'' "yasiyogawiwa") ni sehemu ndogo ya [[maada]] yenye tabia ya kikemia kama [[elementi]]. Kila kitu duniani hujengwa kwa atomi. Atomi ni ndogo kiasi ya kwamba hazionekani kwa macho hata hazionekani kwa [[hadubini]] za kawaida. Kuna aina nyingi za atomi na idadi za aina hizi tofauti ni sawa na elementi zilizopo duniani.
 
Atomi ya [[haidrojeni]], [[oksijeni]] au [[chuma]] ni sehemu kabisa ya elementi hizi. Lakini atomi yenyewe hufanywa na sehemuvyembe ndogovidogo zaidi hasa [[protoni]], [[neutroni]] na [[elektroni]]. Sehemu hizi ndogo zaidi hazina tabia ya elementi fulani ila tu atomi yote ni elementi. Atomi zinatofautiana kutokana na idadi tofauti ya vyembe hivi vidogo ndani yao.
 
== Muundo wa atomi ==
Atomi ni ndogo kiasi ya kwamba hazionekani. Kwa sababu hiyo wataalamu waliunda vielelezo mbalimbali vinavyojaribu kuunganisha tabia mbalimbali za atomi zinazopimiwa.
 
Kielelezo cha [[Ernest Rutherford]] kinasema ya kwamba kwamba katikati ya atomi kuna kiini chenye sehemu kubwa ya mada ya atomi yote. [[Kiini cha atomi]] hufanywa na [[protoni]] na [[neutroni]].
 
Kiini huzungukwa na ganda ambalo ni si dutu imara lakini nafasi ya njia ambako elektroni huzunguka kiini. Nafasi hizi huitwa [[mizingo elektroni]]. Kielezo hiki kimekuwa msingi wa vielelezo vingine kama kile cha Bohr.
 
Kiini huitwa kwa lugha ya Kilatini (pia kiingereza) "nucleus" na hapa lugha ya Kiswahili imepokea neno "nyuklia" kutoka ing. "nuclear" kwa ajili ya mambo yanayohusu matumizi ya nguvu ya atomi, kwa mfano [[nishati ya nyuklia]].
 
== Chaji na ioni ==