Mpira wa kikapu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'thumb|right|Mpira wa kikapu {{Sports}} '''Mpira wa kikapu''' ni mchezo unaopendwa katika sehemu nyingi za dunia. Mara nyingi mchezo...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 09:23, 23 Oktoba 2014

Kigezo:Sports Mpira wa kikapu ni mchezo unaopendwa katika sehemu nyingi za dunia. Mara nyingi mchezo hufanywa ukumbini wakati timu bili za wachezaji wanajaribu kutupa mpira katika kikapu cha timu nyingine. Vikapu viko mwishoni upande mwembamba wa uwanja kwa urefu wa mita 3.05.

Mpira wa kikapu

Kila timu huwa na wachezaji 5 uwanjani na hadi wachezaji wa kando 7 walio tayari kuchukua nafasi ya mchezaji wingine muda wowote. Kila goli katika kikapu cha upande mwingine inahesabiwa kama pointi 2 au 3a kutegemeana na umbali wa kurusha. Goli ya penalti huleta pointi 1.


Historia

Mchezo huu ulianzishwa mwaka na mwalimu James Naismith kwenye chuo cha Springfield College huko Massachusetts. Alibuni mchezo kwa ajili ya wanafunzi wake ili wapate mazoezi wakati wa kipupwe waliposhindwa kucheza nje.

Mpira wa kikapu ulienea haraka kwenye vyuo vya Marekani, katika karne ya 20 pia nje ya vyuoni. 1936 mchezo huu ulikubaliwa kwenye michezo ya olimpiki.

Hadi leo ligi muhimu zaidi duniani ni Chama cha Mpira wa Kikapu Marekani.

 
Vipimo vya uwanja wa mpira wa kikapu

Kanuni za mpira wa kikapu

Shabaha ya mchzo ni kushinda vikapu vingi kuliko timu nyingine.

Mpira unaotumiwa kimataifa ni mpira wa ngozi au mata sintetiki mwenye kipenyo cha milimita 749 hadi 780 na uzito wa gramu 567 hadi 650.

Uwanja huwa na vipimo vya mita 28 kwa 15.

Wakati wa mchezo kuna marefa 2-3 uwanjani. Kando la uwanja hukaa waamuzi wengine wanaoshika wakati na miniti za goli na makosa.

Viungo vya Nje

  • FIBA, Fédération Internationale de Basketball / International Basketball Federation
  • IWBF, International Wheelchair Basketball Federation


 
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: