Utetezi wa Kanisa Katoliki : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d {{mergeto}}
No edit summary
Mstari 2:
{{Kanisa Katoliki}}
 
'''Utetezi wa Kanisa Katoliki''' ni sehemu ya [[teolojia]] ya [[Ukristo]] inayolenga kutoa hoja za kutetea [[imani]] na maisha ya [[Kanisa Katoliki]] dhidi ya zile za watu wa [[madhehebu]] au [[dini]] nyingine au za wale wasio na dini yoyote wanaolenga kuthibitisha kasoro zake.
 
Kwa utetezi wa namna hiyo katika [[lugha]] nyingi limetoholewa neno la [[Kigiriki]] ἀπολογία, apologia, "utetezi wa sauti, hotuba ya utetezi"<ref>{{cite web|title=ἀπολογία|url=http://www.blueletterbible.org/lang/lexicon/lexicon.cfm?Strongs=G627|work=Blue Letter Bible-Lexicon|accessdate=7 May 2012|unused_data=<!-- Replace with BDAG when possible -->}}</ref>.
 
Ni tofauti kidogo na hoja zinaotumiwa na Wakatoliki dhidi ya dini, madhehebu na [[itikadi]] nyingine ili kuonyesha vilivyo na kasoro<ref>{{cite book|last=Kahlos|first=Maijastina|title=Debate and Dialogue : Christian and Pagan Cultures c. 360-430|year=2007|publisher=Ashgate|location=Aldershot|isbn=0-7546-5713-2|pages=7–9}}</ref><ref>{{cite book|last=Ernestine|first=van der Wall|title=Religious Polemics in Context|year=2004|publisher=Royal Van Gorcum|location=Assen|isbn=90-232-4133-9|editor=T L Hettema and A van der Kooij|chapter=Ways of Polemicizing: The Power of Tradition in Christian Polemics}}</ref>
 
==Historia==
Mstari 16:
Baadaye kazi hiyo iliendelezwa na [[walimu wa Kanisa]] wa [[Karne za Kati]], kama vile [[Anselm wa Canterbury]], [[Thoma wa Akwino]] na wengineo wa [[Teolojia ya shule]].
 
Juhudi za pekee zilihitajika na kufanyika wakati wa [[Matengenezo ya Kiprotestanti]], yaliyoelekea kusambaratisha [[Kanisa]] kwa msingi wa [[ufafanuzi]] mpya wa [[Biblia]] na kwa kutegemea [[itikio]] la wengi dhidi ya ma[[kwazo]] yaliyotolewa na baadhi ya viongozi wa ngazi zote, hata Ma[[papa]]. Wakati huo walijitokeza hasa [[Wajesuiti]] kama vile [[Petro Kanisi]] na [[Roberto Bellarmino]].
Wakati wa [[Falsafa ya mwangaza]] kati ya watetezi wa [[Kanisa]] dhidi ya [[falsafa]] hiyo anakumbukwa hasa [[Blaise Pascal]] na katika karne za mwisho [[Gilbert K. Chesterton]].
 
Wakati wa [[Falsafa ya mwangaza]] kati ya watetezi wa [[Kanisa]] dhidi ya [[falsafa]] hiyo anakumbukwailiyopinga hasakabisa [[Blaise Pascalimani]] nayoyote katikaya karnedini, zaanakumbukwa mwishohasa [[GilbertBlaise K. ChestertonPascal]].
 
Katika karne za mwisho kuna [[walei]] waliongokea Ukatoliki kama [[John Henry Newman]] na [[Gilbert K. Chesterton]] huko [[Uingereza]], [[Scott Hahn]] na [[mke]]we huko [[Marekani]] na wengine wengi.
 
Siku hizi, mbali ya vitabu, ma[[gazeti]], vipeperushi, [[kanda]] n.k., kuna [[tovuti]] mbalimbali za kutetea Kanisa Katoliki, ambazo kati yake labda maarufu zaidi ni ile [[Catholic Answers]].
 
==Mbinu==
[[File:Mother Teresa.jpg|thumb|[[Mama Teresa]] mwaka [[1988]].]]
Watetezi hao na wengineo wametumia hoja za kifalsafa, za ki[[historia]] na za fani nyingine, mbali ya madondoo ya [[Biblia]], kadiri ya hoja zilizotumiwa na wapinzani, ambao pengine wanakanusha mafundisho ya Kanisa, pengine wanalaumu zaidi matendo ya wanakanisa, hasa viongozi.
 
Hata hivyo, utetezi mkuu ni [[utakatifu]] wa maisha ya waamini, ambao kila unapopatikana unakumbusha neno la [[Yesu]] kwamba ma[[tunda]] yanathibitisha ubora wa [[mti]] kuliko hoja za [[akili]]. Kati ya hao kuna waamini milioni 30 hivi waliofia dini yao huku wakisamehe watesi wao.
 
==Ugumu wa kazi hiyo==
Ugumu wa kutetea Kanisa hilo una sababu mbalimbali.
 
Upande wa imani na [[maadili]], ni kwamba Kanisa Katoliki lina mafundisho mengi sana kutokana na juhudi za miaka 2000 hivi za kuwa na [[uwiano]] kati ya mitazamo inayopingana. Kanisa hilo halikubali kurahishisha mafundisho kwa kusisitiza upande mmoja unaoeleweka zaidi na kuweka kivulini upande wa pili. Hivyo, kwa mfano, unakiri kuwa Yesu ni [[Mungu]] kweli na papo hapo mtu kweli katika [[umoja]] wa [[nafsi]] yake. Kufafanua [[fumbo]] hilo kwa mtu asiyesadiki ni jambo gumu kuliko kumueleza kwamba ni Mungu tu au mtu tu.
 
Tena, katika [[ulimwengu wa kisasa]], Kanisa Katoliki linajikuta [[mstari wa mbele]] katika kutetea [[uhai]] na [[haki]] duniani, pamoja na kupinga maovu mbalimbali yaliyoenea kwa faida kubwa ya kiuchumi ya makundi mbalimbali. Hivyo si ajabu kwamba linakabiliana na [[chuki]] na [[upinzani]] mkubwa.
 
Upande wa maisha, ugumu ni kwamba Kanisa Katoliki linakaribia kutimiza miaka 2000 ya uwepo wake, likiwa na [[muundo]] unaoonekana, ulioenea sasa duniani kote. Ndani yake hadi sasa wameishi [[bilioni]] kadhaa za [[Wakristo]], wakiwemo [[milioni]] kadhaa za [[wakleri]] na [[watawa]] katika [[mazingira]] mbalimbali, pengine machafu na ya kikatili sana.
 
Kwa kuwa hao pia ni [[binadamu]], si ajabu kwamba kati yao wengine walishindwa [[uaminifu]], lakini ni rahisi kuwanyoshea kidole ili kulaumu Kanisa lenyewe. Yesu alikuwa amesema kwamba [[adui]] yake atapanda [[magugu]] kati ya [[ngano]] aliyosia yeye [[shamba]]ni mwake. Pamoja na hayo, maovu yanazidi kukwaza watu wasiamini. Ingekuwa rahisi zaidi kutetea kundi dogo lililoanza juzijuzi tu.
 
==Maelekezo ya kisasa==
"Tunahitaji utetezi wa aina mpya, kulingana na madai ya leo, ambayo izingatie kwamba jukumu letu si kushinda hoja, bali kuokoa watu, ni kuwajibika katika mapambano ya kiroho, si katika mabishano ya nadharia, ni kutetea na kukuza Injili, si sisi wenyewe".<ref>[[Papa Yohane Paulo II]], hotuba kwa MaaskofuMa[[askofu]] wa [[Karibi]], [[7 Mei]] [[2002]]</ref>
 
==Tanbihi==
{{Reflist|2}}
 
==Viungo vya nje==
*[http://www.catholic.com/ Catholic Answers] (tovuti rasmi)
*[http://forums.catholic.com/ Catholic Answers' forums]
*[http://oce.catholic.com/ Catholic Answers' Original Catholic Encyclopedia]
*[http://www.chastity.com/ chastity.com] Utetezi wa usafi wa moyo
 
{{mbegu-Ukristo}}