Posta ya Kijerumani Lamu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
(Hakuna tofauti)

Pitio la 10:51, 16 Novemba 2014

Posta ya Kijerumani katika mji wa Lamu, Kenya ni jengo la kihistoria na makumbusho ya kipindi cha ukoloni wa Kijerumani kwenye pwani la Kenya.

Mfano wa sare ya wafanyakazi kwenye makumbusho ndani ya jengo la Posta ya Kijerumani mjini Lamu

Jengo hili likasimikwa kama posta ya Dola la Ujerumani tarehe 22 Novemba 1888. Lamu haikuwa eneo la Kijerumani lakini ilikuwa bandari ya pekee iliyotembelewa na meli za Kizungu katika sehemu hii ya pwani. Zaidia ya hayo Lamu ilikuwa jirani na eneo la Usultani ya Witu ambayo iliwahi kuingia katika uhusiano wa ulinzi na Ujerumani tangu 1885.

Mradi wa kikoloni wa Kijerumani katika Witu ilianzishwa na Clement Denhardt ni yeye aliyeanzisha pia posta Kam kisiwani.

Posta hii ilifanya kazi kwa mufa mfupi tu kwa sababu mwaka 1890 Ujerumani ilikabidhi eneo la Witu kwa Uingereza na ofisi ikafungwa 3 Machi 1891.