Tofauti kati ya marekesbisho "Majadiliano ya mtumiaji:Rberetta"

Jibu
(→‎Kazi ya kufanya: mjadala mpya)
(Jibu)
 
Rberetta salaam. Tunafurahi sana kwamba umeanzisha kurasa kuhusu mamalia. Ni kweli, bado hakuna kurasa nyingi kuhusu wanyama wasiotokea Afrika. Lakini, isipokuwa wanyama wanaojulikana sana, nafikiri hiyo si kipaumbele. Ningependa unisaidie kumaliza kurasa kuhusu wanyama wa Afrika na kuandika nyingine mpya. Waafrika waelewe wanyama wao kwanza (siku hizi wengi hawajui majina kwa lugha zao wenyewe). Kwa sasa mimi ninashughulikia kurasa kuhusu arithropodi. Ukikubali nitakushukuru sana. '''[[Mtumiaji:ChriKo|ChriKo]] ([[Majadiliano ya mtumiaji:ChriKo|majadiliano]])''' 15:24, 7 Desemba 2014 (UTC)
:<p>Ndiyo ChriKo, nipo tayari kukusaidia na kazi yako, lakini ningependa kuendelea na nia yangu pia! Labda asilimia 50/50?</p>
:<p>Kwanza, kuhusu kazi yako: Mimi sina ujuzi wa wanyama wa arithropodi kamwe, hata istilahi ya sehemu za miili yao kwa Kiingereza sijui! Lakini, ukitaka nifanye kazi kutafsiri kurasa za arithropodi kutoka Kiingereza, ninafurahi kujaribu kufanya hivyo. Baada ya mimi kumaliza tafsiri, lazima uangalie kazi yangu na kufanya maharirio. Kwa hivyo nitajifunza na kuendelea kuboresha Kiswahili changu. Badala yake, ningeweza kutafsiri kurasa za mamalia ambazo sasa ni mbegu. Bado ningeomba uangalie kazi yangu. Ukiwa na kurasa mahususi ambazo ungependa niziangalie kutafsiri, au kazi nyingine, tafadhali niambie.</p>
:<p>Kuhusa nia yangu, tafadhali nipe nafasi kueleza. Zingatia wanafunzi wanaovutiwa na biolojia. Labda wameona mfumo wa uainishaji wa kibiolojia, na wanastaajabu sana. Mimi ninasikitika kidogo kwamba hao wanafunzi watavumbua mti wa uainishaji (kwa Kiswahili tu), na wataona kwamba matawi mengi yapo matupu katika Wikipedia. Kwa hiyo, nia yangu ni kuanzisha ukurasa mmoja tu katika kila jenasi iliyo tupu sasa hivi. Najua tuna shida za kuchagua majina, na labda kuna wachache wanaojali kuhusu wanyama hawa, hasa ambao hawawezi kusoma lugha nyingine, lakini nina hamasa kuwasaidia hata wachache.</p>
:<p>Pia, nia yangu ni kuleta Vigezo vingine vya oda za mamalia ambavyo havijatafsiriwa bado, kama [[Kigezo:Carnivora]], na kufanya kawaida kurasa nyingi na kuboresha upangaji wao. Wewe na wengine wa jamii mmefanya kazi nyingi sana hapa, lakini vitu vingi vinahitaji uhariri, na nafikiri mimi ndiye mhariri mzuri kuliko mwandishi. '''[[Mtumiaji:Rberetta|Rberetta]] ([[Majadiliano ya mtumiaji:Rberetta#top|majadiliano]])''' 19:58, 7 Desemba 2014 (UTC)</p>
477

edits