Yosefu wa Arimataya : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika '250px|thumb|Yosefu wa Arimataya alivyochorwa na [[Pietro Perugino.]] '''Yosefu wa Arimataya''' alikuwa Myahudi mwanamume...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 07:30, 10 Januari 2015

Yosefu wa Arimataya alikuwa Myahudi mwanamume wa karne ya 1, maarufu hasa kutokana na habari zake zinazopatikana katika Injili (Mk 15:42-46; Math 27:57-60; Lk 23:50-53; Yoh 19;38-42).

Yosefu wa Arimataya alivyochorwa na Pietro Perugino.

Habari za ziada, lakini si za kuaminika, zinapatikana katika vitabu ambavyo havimo katika Biblia ya Kikristo, hasa Injili ya Nikodemu.

Tajiri na mtu wa baraza la Israeli, alichukua jukumu la kumzika Yesu Kristo, akiomba ruhusa ya Ponsyo Pilato na kujitolea kaburi alilokuwa amejiandalia pangoni kwenye Kalivari.

Anaheshimiwa kama mtakatifu na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi, Waanglikana, Walutheri na madhehebu mengine ya Ukristo.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 31 Agosti au nyingine.

Yosefu akimuomba Pilato ruhusa ya kumzika Yesu, kadiri ya James Tissot.

Tanbihi

Viungo vya nje

 
WikiMedia Commons