Bonaventura wa Bagnoregio : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
fix
Mstari 47:
Ulimwengu wote unatangaza [[upendo]] wa Mungu mwema, na maisha ya [[binadamu]] ni safari ya kumuendea. Lakini hawawezi kupanda kwake kwa [[nguvu]] zao bila kuvutwa naye. Ndiyo sababu sala ni ya lazima kama [[mama]] na [[chanzo]] cha kwenda juu.
 
Karibu na mwisho aliandika: “Ukitaka kujua jinsi mambo hayo yote yanavyotokea, uiulize [[neema]], si elimu; uiulize [[hamu]], si [[akili]]; uuulize [[mlio]] wa sala, si [[juhudi]] ya kusoma; umuulize bwanaarusi, si mwalimu; umuulize Mungu, si mtu; uuulize [[ukungu]], si [[weupe]]; usiulize [[mwanga]], bali [[moto]] unaowasha [[nafsi]] yote na kuizamisha ndani ya Mungu kwa [[mpako]] wake tamu sana na ma[[pendo]] motomoto zaidi”.
 
Mashambulizi ya kutisha yalitokea pia ndani ya shirika, upande wa ndugu “wa Kiroho” walioelekea kufuata [[uzushi]] wa [[abati]] [[Yohakimu wa Fiore]], aliyefariki mwaka [[1202]], baada ya kutabiri [[umonaki]] mpya utakaoleta hali mpya katika Kanisa na [[jamii]]. Hao walidhani Ndugu Wadogo ndio waliotimiza [[utabiri]] huo wakajiona hawahitaji tena kuwa chini ya miundo ya zamani, wala chini ya uongozi wa shirika na wa Kanisa, kinyume cha [[utiifu]] mnyenyekevu wa Fransisko.