Ufuaji metali : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika ''''Ufuaji metali''' (ing. ''metallurgy'') inamaanisha jumla ya mbinu za kushughulikia metali na elimu yake. Inahusika pia na aloi ambazo ni mchanga...'
 
No edit summary
Mstari 5:
Halafu inaangalia namna ya kuchanganya na kuunganisha metali mbalimbali kuwa aloi na tabia zake.
 
==Ufuaji metali katika historia ya bindamu==
Historia ya binadamu ina mifano mingmingi jinsi gani maendeleo katika ufuaji metali yalikuwa msingi wa maendeleo ya kijamii. Hapo ndipi sababu ya kupanga historia kwa awamu za [[Zama za Mawe]], [[Zama za Shaba]] na [[Zama za Chuma]].
 
Kabla ya kupatikana kwa matumizi ya metali watu walitumia vifaa vya jiwe, ubao au mfupa kwa kurahisisha shughuli za kila siku. Vifaa hivi vinakosa ugumu sawa na metali kwa hiyo havidumu sana ingawa vinaruhusu utekelezaji wa kazi nyingi.
 
Metali ya kwanza iliyotumiwa na watu ilikuwa [[dhahabu]] <ref>[http://www.gold-eagle.com/article/history-gold History of Gold]</ref> pamoja na [[shaba]] maana metali hizi zinaweza kupatikana safi kiasili na ni laini ya kutosha. Zinaweza kupewa umbo kwa kuzipiga na hivyo vipambio vya dhahabu na shaba ni vifaa vya kimetali vya kwanza vilivyotengenezwa na binadamu. Ushuhuda wa kale wa teknolijia ya ufuaji shaba ni wa mnamo mwaka [[5,000 KK]] huko Serbia.<ref>[https://www.sciencenews.org/article/serbian-site-may-have-hosted-first-copper-makers "Serbian site may have hosted first copper makers", kuhusu ugunduzi wa ufuaji shaba miaka 7000 iliyopita huko Serbia]</ref>
 
Haijulikani jinsi gani watu walivyotambua njia za kupasha moto metali na madini ya metali lakini kuna uwezekano ya kwamba maendeleo haya yalikuja pamoja na teknolojia ya [[ufinyanzi]] wakati vyungo vilichomwa na joto ndani ya majiko lilisababisha kuyeyuka kwa metali ndani ya udongo au mawe yaliyotumiwa kutengeneza jiko.
 
Ilhali dhahabu ni laini mno tayari shaba inafaa kutumiwa kwa vifaa kama visu au silaha nyingine pamoja na vipambio. Lakini shaba peke yake ina hasara mbili: si gumu sana yaani umbo lake halidumu likitumiwa kwa kazi zito au kwa mapigano; ukali wa kisu au shoka inapotea haraka. Hasara nyingine inafanya mmenyuko na oksijeni ya hewa au katika maji na uso wake hubadilika kuwa ganda la oksaidi.
 
Baada ya karne kadhaa za zama za shaba watu waligundua njia ya kuboresha ugumu wa shaba kwa kuichanganya na [[stani]] na hivyo kupata aloi ya [[bronzi]] (shaba nyeusi). Hii ilikuwa aloi ya kwanza inayojulikana kuwa ilitumiwa na binadamu katika historia yake. Shoka na vyembe vya bronzi viliboresha shughuli za kila siku, silaha za bronzi ziliongeza nguvu ya wanajeshi.
 
Ilichukua tena karne kadhaa hadi watu wa kwanza waligundua njia za kutumia chuma ambacho kinazidi ugumu wa shaba na bronzi. Kuna dalili kuwa Wahittiti katika Asia Ndogo walikuwa watu wa kwanza waliogundua teknolojia hii. Watu wenye silaha za chuma na feleji waliweza kuwashinda wapinzani waliotumia silaha za bronzi kwa sababu ukali wa upanga wa chuma unazidi ule wa bronzi.
 
 
== Kupata metali kutoka mashapo ==