Mzee : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Enock John
 
No edit summary
Mstari 1:
'''Mzee''' ni mtu aliyeishi miaka mingi baada ya kuzaliwa.
 
Katika jamii za kiafrika sawa na jamii nyingi duniani neno "mzee" linatumiwa pia kama cheo cha heshima kwa kumtaja mtu mwenye mamlaka fulani. Hapo kuna hoja la kuwa mtu aliyeendelea katika umri anawazidi vijana kwa hekima na maarifa pia kwa hiyo anafaa kutawala au kufanya maazimio au angalau kutoa ushauri.
 
Matumizi ya kulingana ya maneno yenye maana ya "mzee" yanapatikana kwa lugha mbalimbali
* neno '''sheikh''' (‏شيخ‎) kwa Kiarabu kiasili linamtaja mtu mwenye umri wa juu, leo imekuwa neno la kutaja watawala, wakuu wa kabila fulani au pia viongozi wa makundi ya kidini ya Kiislamu.
* "[[Senati]]" katika mfumo wa kisiasa wa nchi mbalimbali ni kitengo cha [[bunge]]. Neno latokana na lugha ya Kilatini "senatus" ambako kiasili lilitaja mkutano wa wazee. Katika Kilatini neno latokana na "Senex" yaani mtu mwenye umri mkubwa.