Mzee : Tofauti kati ya masahihisho

1,628 bytes added ,  miaka 8 iliyopita
no edit summary
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 3:
Katika jamii za kiafrika sawa na jamii nyingi duniani neno "mzee" linatumiwa pia kama cheo cha heshima kwa kumtaja mtu mwenye mamlaka fulani. Hapo kuna hoja la kuwa mtu aliyeendelea katika umri anawazidi vijana kwa hekima na maarifa pia kwa hiyo anafaa kutawala au kufanya maazimio au angalau kutoa ushauri.
 
==Mzee katika jamii==
Kimapokeo tamaduni nyingi duniani zinajua heshima ya mzee. Hapo kiongozi anateuliwa kati ya wazee. Halmashauri ya wazee ni bodi ya kufanya maazimio muhimu. Mkutano wa wazee ni mahali pa kuchukua rufaa kwa hiyo ina kazi inayolingana na mahakama kuu katika jamii zenye taasisi hizi.
 
Wazee ni watu wanaotunza mila na desturi pamoja na kumbukumbu ya historia na wanapaswa kusikilizwa kwa heshima.
<ref>Elders were and are the guardians of the culture, traditions, and history of the people. Integrity, generosity, wisdom, articulateness, subtlety, patience, tactfulness, gratefulness, and being listened to and respected by others are all qualities of an Elder. [http://www.africanholocaust.net/ritesofpassage.html#elder Elder Roles]</ref>
 
Katika jamii zilizopangwa kwa [[rika]] (vikundi kulingana na umri) kama Wamasai au [[Wazulu]] rika ya wazee inapaswa kusikilizwa katika maazimio yanayohusu jamii yote.
 
Wakati umri unazidi na wazee wanakuwa wadhaifu ugumu unaanza kuendelea na cheo cha heshima. Hata hivyo wote wanapaswa kuonyesha heshima kwao hata kama hali halisi hawatafuri tena ushauri wao. Tatizo hili ni tofauti kati ya tamaduni za kimila ambako watu wadhaifu hawaishi muda mrefu sana kutokana na uhaba wa nafasi za tiba upande mmoja na tamaduni zilizoendelea ambako nafasi a tiba zinawezesha watu wengi kufikia umri mkubwa ambako asilimia inaanza kupoteza akili au uwezo wote wa kutembea kwa miaka mfululizo. <ref>[http://faculty.usfsp.edu/jsokolov/webbook/fry.pdf Culture and the Meaning of a Good Old Age]</ref>
 
==Mzee katika tamaduni mbalimbali==
Matumizi ya kulingana ya maneno yenye maana ya "mzee" yanapatikana kwa lugha mbalimbali
* neno '''sheikh''' (‏شيخ‎) kwa Kiarabu kiasili linamtaja mtu mwenye umri wa juu, leo imekuwa neno la kutaja watawala, wakuu wa kabila fulani au pia viongozi wa makundi ya kidini ya Kiislamu.
* "[[Senati]]" katika mfumo wa kisiasa wa nchi mbalimbali ni kitengo cha [[bunge]]. Neno latokana na lugha ya Kilatini "senatus" ambako kiasili lilitaja mkutano wa wazee. Katika Kilatini neno latokana na "Senex" yaani mtu mwenye umri mkubwa.
 
==Marejeo==
<references/>
 
[[Jamii:Cheo]]