Tofauti kati ya marekesbisho "Atomu"

351 bytes added ,  miaka 7 iliyopita
No edit summary
Atomi ni ndogo kiasi ya kwamba hazionekani. Kwa sababu hiyo wataalamu waliunda vielelezo mbalimbali vinavyojaribu kuunganisha tabia mbalimbali za atomi zinazopimiwa.
 
Kielelezo cha [[Ernest Rutherford]] kinasema ya kwamba kwamba katikati ya atomi kuna kiini chenye sehemu kubwa ya madamaada ya atomi yote. [[Kiini cha atomi]] hufanywa na [[protoni]] na [[neutroni]]. Atomi za elementi ileile zinaweza kutofautiana katika idadi ya nyutroni ndani ya kiini na hali hizi tofauti huitwa [[isotopi]] za elementi. Isotopi tofauti ya elementi moja zinapangwa kwenye nafasi ileile ya [[jedwali la elementi]]. Isotopi kadhaa si thabiti lakini [[nururifu]] yaani zinaweza kutoa vyembe au nururisho na kuhamia elementi nyingine.
 
Kiini huzungukwa na ganda ambalo ni si dutu imara lakini nafasi ya njia ambako elektroni huzunguka kiini. Nafasi hizi huitwa [[mizingo elektroni]]. Kielezo hiki kimekuwa msingi wa vielelezo vingine kama kile cha Bohr.