Uhai : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika ''''Uhai''' kwa maana ya biolojia ni jumla ya tabia zinazotofautisha kiumbehai na maada kwa jumla. Kila uhai ulioweza kutazamiwa na sayansi unapatikana p...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 12:59, 27 Aprili 2015

Uhai kwa maana ya biolojia ni jumla ya tabia zinazotofautisha kiumbehai na maada kwa jumla. Kila uhai ulioweza kutazamiwa na sayansi unapatikana pamoja na maada.

Kati ya tabia hizi ni uwezo wa kushawishika na mazingira, kujipanga, kukua, metaboli na kuzaa. Kila tabia pekee yake haifanyi uhai kwa sababu moja-moja zinaweza kutokea pia kwa mata isiyo hai: fuwele zinakua, ulimi wa moto ina umbo maalumu na ndani yake kuna aina ya metaboli inayobadilisha molekuli za nta pamoja na oksijeni ya hewani dioksidi kabonia na maji. Kwa hiyo ni jumla ya tabia lakini kwa sababu kuna tofauti kati ya viumbehai ambazo hazifanani katika tabia zote wka pamoja kumbe hadi leo wataalamu hawakupatana bado ni masharti gani yanayohitaji kuwepo kwa "uhai".

Uhai unpatikana kwa umbo la viumbehai vinavyopangwa katika vikundi vinavyofanana kati yao. Kila kiumbehai hufanywa na vitengo hai ndani yake vinavyoitwa seli.