Burundi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 116:
Katika Burundi kikosi cha kwanza cha Kijerumani kilifika mnamo [[1896]] wakakuta ufalme wa mwami wakaridhika kumwacha mwakilishi mkazi (resident) katika [[mji mkuu]] [[Gitega]] ambaye hakuhusika na mambo ya utawala wa ndani. Wakati ule eneo lilijulikana kwa jina "Urundi". Hapa sawa na Rwanda na [[Bukoba]] Wajerumani walitumia [[mbinu]] ya [[eneo lindwa]] ingawa walikuwa pia na majadiliano kuingiza falme hizi za kienyeji moja kwa moja ndani ya koloni lao.
 
Baada ya [[Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia]] Burundi pamoja na Rwanda ilikabidhiwa kwa [[Ubelgiji]] kwa niaba ya [[Shirikisho la Mataifa]] kama [[eneo la kudhaminiwa] lililoitwa Ruanda-Urundi. Kimsingi Wabelgiji waliendelea na mfumo wa Wajerumani uliomwachia mtemi [[mamlaka]] kubwa. Waliweka Ruanda-Urundi chini ya serikali ya Kongo ya Kibelgiji.
 
Lakini baadaye walianza kuingilia zaidi na ilhali wakati ule walipendelea Watutsi karibu na machifu wote walikuwa Watutsi na Wahutu walipotea katika nafasi za uongozi kimahali.
 
Tangu 1946 Shirikisho la Mataifa lilikwisha na Ubelgiji ilipokea wito wa kutawala Ruanda-Urundi na [[Umoja wa Mataifa]]. Mwaka 1 kabla ya uhuru kulikuwa na uchaguzi wa kwanza chini ya usimamizi ya [[UM]] na chama mshindi ilikuwa UPRONA iliyoongozwa na mwanamfalme Mtutsi [[Louis Rwagasore]] aliyemwoa mke wa Kihutu na chama kiliunganisha pande zote mbili. Lakini miezi michache Rwgasore aliuawa na chama chake kilitengana kufuatana na ukabila.
 
1962 Umoja wa Mataifa uliamua kuipa Ruanda-Urubdi uhuru kamili, lakini kila nchi pekee.
 
Baada ya uchaguzi wa 1965 mapigano yalitokea kwa silaha, na kikundi cha Watutsi wakali kilichukua serikali. 1966 mwami alipinduliwa na mwanasiasa Michel Micombero aliyejitangaza kuwa rais na nchi kuwa jamhuri. Kuanzia sasa wanasiasa na watumishi wakubwa walio wahutu walifukuzwa, kukamatwa au kuuawa.
 
== Utawala ==