Vita Kuu ya Pili ya Dunia : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d Removing Link FA template (handled by wikidata) - The interwiki article is not featured
Mstari 12:
Mwezi wa Aprili 1940 Waingereza walianza kupeleka wanajeshi '''[[Norway]]''' wakiwa na shabaha ya kuzuia kupelekwa kwa madini ya chuma kutoka [[Sweden]] kwenda Ujerumani kupitia mabandari ya Norway. Wajerumani walichukua nafasi hii kuteka '''[[Denmark]]''' na Norway na kufukuza Waingereza.
 
'''Mei [[1940]] Wajerumani walishambulia Ufaransa''' pamoja na nchi za [[Uholanzi]], [[Ubelgiji]] na [[Luxemburg]]. Vita hii ilikwisha haraka Wajerumani walishinda na kupiga pia kikosi cha Waingereza huko Ufaransa. Baadaye walisitasita kushambulia Uingereza peyeweyenyewe. Mipango yao ilihitaji mbinu za kuvuka bahari. Wakajaribu kuvuruga nguvu ya kijeshi ya Waingereza kwa mashambulizi ya ndege lakini hawakuwa na uwezo wa kutosha. Katika shambulizi dhidi ya Ufaransa Waitalia walishirikiana kwa upande wa Wajerumani.
 
Mwisho wa 1940 Waitalia walianza kuwashambulia [[Ugiriki]] na jeshi la [[Uingereza|Waingereza]] huko [[Misri]] na [[Malta]]. Lakini mahali pote walirudishwa nyuma hadi kiongozi Mjerumani [[Adolf Hitler]] aliamua kuwasaidia Waitalia na kupeleka wanajeshi Wajerumani kwenda [[Afrika ya Kaskazini]] pamoja na Ugiriki mwaka [[1941]]. Hii ilisababisha pia Wajerumani kuteka [[Yugoslavia]] wakiwa njiani kwenda Ugiriki.