Tofauti kati ya marekesbisho "Jicho"

2 bytes added ,  miaka 6 iliyopita
d (→‎Macho ya mamalia: All info is kept in Wikidata, removed: {{Link FA|an}} using AWB (10903))
Kuna mifumo mbalimbali ya macho kati ya aina mbalimbali ya [[wanyama]].
 
Macho ya kimsingi kwa viumbehai vidogo yanatambua tu kama mazingira inayana mwanga au la. Hata kati ya wenye seli moja hu kuna viumbehai vyenye protini zinazotofautisha giza na nuru. Kuna konokono ambao hawawezi "kuona" picha ya mazingira lakini wanatambua mwanga na uwezo huu unawawezesha kuepukana na mwanga wa jua ambako wangekauka.
 
Macho yaliyoendelea kiasi yana umbo kama kikombe na hii inawezesha kutambua ni upande gani nuru inapotokea.
Wanyama wengi huwa na macho yaliyoendelea zaidi yana uwezo wa kuona picha halisi ya mazingira pamoja na rangi na mwendo.
[[Picha:Drosophilidae_compound_eye.jpg|thumb||Jicho la inzi (drosophila) chini ya hadubini; lenzi ya kila omatidi inaonekana kama nusu tufe]]
 
== Macho ya kuungwa ==
[[Wadudu]] na [[arthropoda]] hua na [[macho ya kuungwa]] na vijicho vingi vidogo vinavyoitwa omatidi; kila kijicho huwa na umbo la kijiti na kwenye mwisho wake kuna lenzi ya chitini. Mdudu anaweza kuwa na vijicho vielfu na picha ya mazingira inaunganishwa na picha nyingi ndogo za kila kijicho. Macho haya ya kuungwa yanamwezesha mdudu kuangalia asilimia kubwa ya mazingira yake kwa aina kadhaa hata nyuma yake. Macho ya kuungwa yanaweza kufunika hadi asilimia 80 ya eneo la kichwa. Mdudu haoni vikali kama mtu lakini anaona mabadiliko na mwendo haraka sana.